Waziri wa Nchi Ofisi ya Aaziri Mkuu - Uwekezaji, Angela Kairuki akisalimiana na Meneja Mwandamizi wa Wateja wa Serikali wa Benki ya CRDB, Nuru Kateti alipotembelea Banda la CRDB, baada ya kufungua Kongamano la wawekezaji mkoani Songwe lililoandalia na Mkuu wa Mkoa huo, Brig. Jenerali Mstaafu, Nicodemus Mwangela kwa kushirikiana na wadau mbalimbali katika juhudi za kukuza na kuleta chachu ya maendeleo ya uwekezaji mkoani songwe. Kulia ni Meneja wa Benki hiyo Kanda Nyanda za Juu Kusini, Denis Mwoleka.
Waziri Kairuki aliipongeza benki ya CRDB kwa kuwa mdau mkubwa katika kuleta chachu ya maendeleo nchini kwakuwa mstari wa mbele kuhakikisha inawawezesha wadau na sekta mbalimbali kwa kutoa mikopo ya uwekezaji. Aidha aliwataka wawekezaji Songwe na nchini kuchangamkia fursa za mikopo zitolewazo na benki hiyo. Benki ya CRDB ni moja ya wadhamini katika kongamano hilo linalofanyika kwa siku tatu ambalo lilitanguliwa na semina elekezi iliyoendeshwa na mkuu huyo wa mkoa Februari 15, 2020 na linatarajia kufikia kilele Februari 17, 2020 katika viwanja vya CCM mjini Vwawa. |
No comments:
Post a Comment