- Wateja wa Vodacom M-Pesa kupokea pesa kutoka zaidi ya nchi 50 duniani kwa kutumia app ya WorldRemit kwa haraka
Huduma hiyo mpya inaongeza urahisi wa wapokeaji wa uhamishaji wa pesa mijini na vijijini kwani wanaweza kupokea pesa kutoka kwa jamaa na marafiki nje ya nchi moja kwa moja kwenye simu zao, bila kuhitaji kuwa na akaunti ya benki au kuunganishwa katika mtandao.
WorldRemit ni mojawapo ya vinara ulimwenguni katika utoaji wa huduma ya uhamishaji pesa kupitia akaunti za simu ya mkononi, ambapo wameunganishwa na akaunti zaidi ya milioni 160 katika nchi 29. Mbali na huduma ya pesa kwa njia ya simu ya mkononi, kampuni hiyo pia inatoa huduma za uhamishaji wa kibenki, huduma ya kuchukua pesa papo hapo na kuongeza muda wa maongezi nchini Tanzania.
Mkurugenzi wa M-Pesa Ltd Epimack Mbeteni alisema, “Ushirikiano huu mpya na WorldRemit utatuwezesha kutambua malipo yanayofanyika kuja nchini Tanzania kila mwaka,utaongeza urahisi na uwezo kwa familia na marafiki nchini Tanzania kupokea pesa kupitia M-Pesa kutoka ulimwenguni kote na kufaidika na huduma za mawakala wetu zaidi ya 106,000 wa M-Pesa kote nchini, pamoja na mfumo wetu wa kibenki, unaowaunganisha na M-Pesa.Hii ni njia mojawapo ya kuboresha maisha ya wateja wetu '
Kwa mujibu wa Benki ya Dunia, mwaka 2017 Wahamiaji wa kiafrika walituma dola bilioni 38 kurudi nyumbani ambapo mwaka huu inakadiriwa kufikia bilioni 39.6. Pesa inayotumwa kwa familia hutumika kuleta maendeleo na kufanya shughuli mbalimbali za kiuchumi. Malipo katika kiwango cha kidunia kwa Tanzania mara nyingi yanafanyika kupitia katika benki, ambapo bado kuna changamoto za gharama za kutuma, utaratibu wa utambulisho na muda unaotumika hadi kupata pesa.
“Ushirikiano huu utatoa suluhisho mbadala kwa kuwepo na wepesi na gharama nafuu katika kupokea pesa kutoka nje ya nchi kwa maana ya familia kupokea pesa moja kwa moja kwenye akaunti zao za M–Pesa na wanaweza kuzitumia kwaajili ya kuleta maendeleo na katika shughuli nyingine za kiuchumi kama akiba na mikopo, huduma ya kutoa pesa zaidi,malipo ya kieletroniki na nyingine nyingi kutoka Vodacom,” aliongeza Epimack.
Kwa kutumia WorldRemit Watanzania wanaoishi katika nchi zaidi ya 50, ambazo ni pamoja na Amerika, Uingereza na Canada huokoa muda wao mwingi na pesa kwani hawahitaji kusafiri kwenda kwa wakala wa kuhamisha pesa na kulipa ada ya kutuma pesa nyumbani. Badala yake wanaweza kutuma pesa kwa njia ya mtandao wakati wowote kwa kutumia zana (app) au tovuti ya WorldRemit.
WorldRemit hailazimiki kulipa gharama zinazohusiana na mawakala wa maeneo katika nchi zinazohusika kutuma pesa, kampuni inapeleka akiba hizi moja kwa moja kwa wateja.
Kwa mujibu wa Benki ya Dunia, gharama ya wastani ya kutuma £120 (~ $ 155) kutoka Uingereza kuja Tanzania ni karibu 9.5%
Gharama ya WorldRemit kwa kiasi kama hicho inaanzia chini ya 2%. Kampuni hiyo pia kwa sasa imeondoa gharama katika miamala mitatu ya kwanza endapo watatumia namba ya utambulisho 3 FREE wanapofanya malipo.
Kwa upande wake, Mkurugenzi wa World Remit ukanda wa Afrika Mashariki na Kati, Sharon Kinyanjui alisema kwamba ushirikiano huu utapunguza ada za kutuma fedha, “uzinduzi huu utapunguza ada ambazo wateja wamekuwa wakilipa, hii ni kwa sababu kila kitu kinafanyika kidijitali,” aliongeza.
Meneja wa WorldRemit Tanzania, Cynthia Ponera, alisema, “Huduma yetu ya kuhamisha pesa kwa Tanzania inakua kwa zaidi ya asilimia 100, mwaka hadi mwaka, na huduma ya pesa kwa njia ya simu ya mkononi ndiyo njia yetu kuu tunayoitumia kutuma pesa nchini.
Tunafurahi kushirikiana na Vodacom kupanua mtandao wetu zaidi na kuwaunganisha wateja zaidi ya milioni 12 wa M-Pesa kwenye huduma yetu ya kuhamisha pesa.Ushirikiano wetu utapunguza gharama ya kutuma pesa nchini na kuunga mkono mipango ya ujumuishaji wa kifedha kwa kuwapa fursa wapokeaji walioko vijijini katika kupata huduma hii rasmi ya uhamishaji pesa huko walipo”, alihitimisha bi. Ponera.
Kwa taarifa zaidi jinsi ya kutuma pesa kwenda Tanzania, bonyeza hapa.
Mawasiliano ya vyombo vya habari
WorldRemit
Jo Bancroft
PR Manager
jbancroft@worldremit.com
Vodacom Tanzania
Alex Bitekeye
PR Manager
bitekeyea@vodacom.co.tz
Kuhusu WorldRemit
WorldRemit imeboresha sekta hii ambayo hapo awali ilimilikiwa na wachache kwa kuipeleka katika anga za kimataifa kwa kutuma hela kwa njia ya mtandao- kwa usalama zaidi, haraka na kwa gharama nafuu. Kwa sasa tunatuma kuanzia katika nchi 50 hadi 150 na kutoa huduma katika vituo 6,500 vya kutuma pesa ulimwenguni kote.
Kwa upande wa utumaji, WorldRemit inatumia mfumo wa malipo wa kidigitali kwa asilimia 100, kuongeza urahisi na usalama.Kwa wapokeaji wa pesa, kampuni inatoa wigo mpana ikiwamo kuweka benki, kuchukua pesa taslimu, kuongeza muda wa maongezi na huduma ya pesa kwa simu ya mkononi.
Ikiungwa mkono na Accel, TCV na Leapfrog - wawekezaji wa awali katika Facebook, Netflix na Slack, makao makuu ya WorldRemit yako London, Uingereza ikiwa ni pamoja na uwepo wa ofisi za kimataifa, Marekani, Canada, Korea Kusini, Japan, Singapore, Ufilipino, Australia na New Zealand.
Kuhusu Vodacom M-Pesa Tanzania
Vodacom M-Pesa ni huduma ya kifedha kwa njia ya simu inayoongoza nchini iliyoanzishwa na Vodacom Tanzania PLC mwaka 2008. Kwa sasa ni moja ya huduma chache duniani zilizopewa tuzo ya ubora ya GSMA na ina wateja zaidi ya milioni 10. Kwa kiasi kikubwa M-Pesa imechangia katika kukua kwa huduma za kifedha na shughuli za uchumi nchini. Wateja wanatuma na kuweka pesa kupitia huduma ya M-Pesa kupitia kwa mawakala zaidi ya 106,000 nchini kote. Mfumo wa M-Pesa unaunganisha mabenki, makampuni na mashirika ya Serikali katika kufanya malipo ya kidigitali.
Kwa sasa, M-Pesa inaendelea kuwa kinara katika soko la huduma za kifedha nchini kupitia huduma zake za kibunifu kama vile Akiba na Mikopo, malipo ya kieletroniki, huduma za vikundi na nyingine nyingi ambazo zinakidhi mahitaji ya watanzania na kuwezesha ufikaji na utumiaji Zaidi wa huduma rasmi za kifedha.
No comments:
Post a Comment