Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na wenye Ulemavu, Mhe. Jenista Mhagama amewataka waajiri nchini, kuhakikisha wanawawezesha wafanyakazi wanokwenda kuhudhuria mafunzo mbalimbali ili waweze kupata ujuzi unaohitajika na utakaokidhi ushindani katika mazingira ya kibiashara.
Mhe. Mhagama ameyasema hayo jijini Dar es Salaam hivi karibuni wakati wa hafla ya utoaji tuzo za waajiri bora wa mwaka kwa mwaka 2019, tuzo zilizoandaliwa na Chama cha Waajiri Tanzania (ATE).
Waziri alisema wafanyakazi wakipata mafunzo hayo watajiongeza ujuzi, watafanya kazi kwa bidii na kuongeza uzalishaji mahali pa kazi kwa lengo la kupambana na mabadiliko ya teknolojia.
"Sisi sote ni mashahidi mabadiliko ya teknolojia ni makubwa kweli kweli, kwa hiyo kama hatutawashirikisha wafanyakazi wetu kupata ujuzi mpya na mafunzo endelevu katika maeneo yetu ya kazi ambayo yatawasaidia kuendana na mabadiliko hayo ya teknolojia katika ulimwengu, tunaweza tukajikuta hatupigi hatua kwenda mbele na hatutaweza kufikia malengo tuliyojiwekea ndani ya taasisi zetu na taifa kwa ujumla," alisema.
Alisema pia anawakumbusha waajiri kuendelea kuchangia katika mfuko wa fidia kwa wafanyakazi kwani umekuwa ukiwakinga waajiri na madhala na majanga wanayoyapata mahali pa kazi.'
Uchangiaji katika mfuko huu una manufaa makubwa situ kwa wafanyakazi hata kwa waajiri kwani utamsaidia mwajiri kuwa na nguvu kazi yenye afya njema itakayo fanya kazi kwa kujiamini," alisema
Aidha alisema wanapoendelea kuijenga nchi hasa katika kuwekeza kwenye sekta ya viwanda wanategemea kwa kiasi kikubwa mchango wa sekta binafsi kama injini ya kujenga uchumi hivyo maamuzi ya ATE ya kutambua na kuwekeza katika rasilimali watu ni kuongeza tija kwenye maeneo ya kazi.
Aidha alisema wao kama serikali, waajiri na Chama cha wafanyakazi nchini (Tucta) watahakikisha kwamba tuzo hizo zinaendelea kila mwaka bila kukoma kwani ni chachu kwa waajiri katika kuleta mabadiriko mahala pa kazi.
Naye Naibu Waziri Ofisiya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Stella Ikupa amewataka waajiri kuendelea kuunga mkono juhudi za serikali katika kuwasaidia watu wenye ulemavu vifaa visaidizi
"Vifaa visaidizi kwa watu wenye ulemavu ni kama chakula maana vinahitajika kila siku.
Unapo mnunulia mtu mwenye ualbino mafuta yataisha na atahitaji mengine baada ya muda hivyo ni muhimu sana kwa wadau kujitokeza kwa wingi kununua vifaa hivyo vikiwamo fimbo kwa wasiyona na Wheel Chair (viti vya walemavu),"alisema
Kwa upande wake Ofisa Mtendaji wa ATE, Agrey Mlimuka alisema tuzo hizo zilianza kutolewa mwaka 2005 zimekuwa zikihamasisha kampuni wanachama kuweka juhudi katika masuala ya ajira na usimamizi wa rasilimali watu kama msingi na mkakati wa kujenga nguvu kazi yenye ujuzi, furaha na ushindani.
Alisema kutokana na mapendekezo yaliyotolewa, kwa mwaka huu tuzo hiyo ya mwajiri bora imeongeza vipengele vipya vitatu hivyo kufanya kuwa na jumla ya vipengele 38 kutoka 35 vilivyokuwepo mwaka jana.
Vipengele vilivyoongezeka ni mwajiri bora anayeendeleza mafunzo ya ujuzi kwa Kazi kwa wahitimu, mwajiri bora anayetoa mafunzo ya uwanangezi pamoja na tuzo ya mwajiri bora anayezingatia haki rasilimali, haya yaliku wamaagizo ya waziri mwakajana na tumeyatekeleza.
Alisema lengo la kuongeza vipengele hivyo nikuendelea kuboresha tuzo hizo, kuongeza ushindani miongoni mwawashiriki pamoja na kugusa kila eneo ambalo litaleta tija katika ukuzaji na uendelezaji warasilimaliwatu katika maeneo ya kazi.
"Tunatambua bila rasilimali watu hatuwezi kupiga hatua wala kwenda kwenye uchumi wa viwanda tunao usema, hivyo tuzo hizo mpya ni nyongeza katika zile zinazotolewa ambazo ni utawala na uongozi, ubora na usimamizi warasilimaliwatu, bidhaa na huduma, uwajibikaji katika mwenendo wa biashara, pamoja na usalama wa mwajiri wakati eneo la kazi”
Alisema wameendelea kuwa na tuzo ya mshindi wa jumla na kuongeza kuwa ushiriki wa kampuni katika tuzo hizo umeendelea kuongezeka mwaka hadi mwaka kutokana na ukweli kwamba ni jambo muhimu kwa ustawi wa wafanyakazi.
Kwa upande wake Mwenyekitiwabodiya ATE, Jayne Nyimbo alisema wanaomba wapate fursa ya kukutana na Rais John Magufuli kwani tangu aingie madarakani hajapata nafasi ya kukutana na waajiri ili kujua changamoto wanazo kumbananazo.
Alisema ATE wanaamini kuwa iliwafikie mafanikio hasa katika Nyanja za kiuchumi na kijamii ni muhimu kuzingatia mgawanyo sawa warasilimali zao nchini kwa watu wote.
"Kwa kuzingatia hilo waajiri tunaendelea kutekeleza program maalum ya Female ambayo inalengo kuwajengea uwezo wanawake na hicho kuwawezesha kushika nafasi za uongozi katika Nyanja mbalimbali katika taifa letu, natoa wito kwa waajiri waendelee kushiri kikatika mpango huu ili kujenga mazingira yanayo jail usawa wa kijinsia hasa katika ngazi za maamuzi," alisema.
No comments:
Post a Comment