Foreign Exchange Rates

DStv Advert_090724

DStv Advert_090724

SBT Tanzania Advert_291123

Tuesday, 12 November 2019

VODACOM TANZANIA IMEONGEZA PATO LAKE KWA ASILIMIA 6.5 KATIKA KIPINDI CHA MIEZI SITA

Vodacom Tanzania PLC imerekodi ongezeko la mapato kwa asilimia 6.5 kufikia shilingi bilioni 528,962 kwa kipindi cha miezi sita.

Ongezeko hili limechagizwa na ukuaji wa wateja wetu wa msingi, ukuaji wa mapato ya M-Pesa na data za simu pamoja na uwekezaji uliolenga kupanua mtandao wetu wa data na kusambaza huduma ya 4G nchini kote na huduma za kifedha kupitia M-Pesa.

Uwekezaji mkubwa wa shilling bilioni 78.7 katika kupanua mtandao wa 4G na kuongeza ubora wa mtandao pia umechangia kuongeza wateja na kufikia milioni 14.8 ambayo ni ongezeko la asilimia 5.5.

Mkuu wa Uhusiano wa Uwekezaji na Miradi Maalumu Vodacom Tanzania Plc, Robin Kimambo akifafanua kuhusu matokeo ya mapato na matumizi ya nusu mwaka ya kampuni hiyo kwa wahariri wa habari za biashara waliohudhuria wakati wa utangazaji matokeo hayo jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki.
Mkuu wa Mipango na Uwekezaji wa Vodacom Tanzania Plc, Hilda Bujiku akifafanua kuhusu matokeo ya mapato na matumizi ya nusu mwaka ya kampuni hiyo kwa wahariri wa habari za biashara waliohudhuria wakati wa utangazaji matokeo hayo jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki.

Mhariri wa gazeti la The Citizen, Mnaku Mbani akiuliza swali kwenye mkutano wa wahariri wa habari za biashara kuhusu matokeo ya mapato na matumizi ya nusu mwaka ya kampuni ya Vodacom Tanzania Plc wakati wa utangazaji matokeo hayo jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki.
Wahariri wakimsikiliza mtoa mada, Robin Kimambo kwenye mkutano wa wahariri wa habari za biashara kuhusu matokeo ya mapato na matumizi ya kampuni ya Vodacom Tanzania Plc wakati wa utangazaji matokeo hayo jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki.
Mkuu wa Mipango na Uwekezaji wa Vodacom Tanzania Plc, Hilda Bujiku akifafanua kuhusu matokeo ya mapato na matumizi ya nusu mwaka ya kampuni hiyo kwa wahariri wa habari za biashara waliohudhuria wakati wa utangazaji matokeo hayo jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki.

No comments:

Post a Comment