Meneja wa Biashara za Nje wa Sachsenküchen, Dominik Shulze Doring akizungumza na wageni na waandishi wa habari waliohudhuria kwenye uzinduzi wa duka jipya la kisasa la vyombo vya jikoni.
|
Akizungumza wakati wa uzinduzi wa moja ya maduka yake Mikocheni, jijini Dar es Salaam, Meneja wa Biashara za Nje wa Sachsenküchen, Dominik Shulze Doring, amesema kwamba ukaribu na wateja utarahisisha kufikisha huduma zao kwa wateja wa Tanzania.
“Kwa kuzindua duka la Sachsenküchen, ikiwa ni la kwanza barani Afrika, tunawaletea Watanzania bidhaa mbalimbali ambazo tunazizalisha. Pia tunaleta huduma za usanifu wa majiko kutokana na mahitaji ya mteja,” Doring ameelezea.
Meneja wa Sachsenküchen –Tanzania, Ronald Harold nae amesema: “Tunafuraha kwa kuweza kushirikiana na watengenezaji wa vyombo vya jikoni wanaotambulika duniani ili kuweza kuleta bidhaa zenye ubora wa hali ya juu kwenye soko. Tanzania pia itafaidika kwa kupata uzoefu na ujuzi watakaoleta washirika wetu kutoka Ujerumani ambao wana uzoefu wa zaidi ya miaka 100”
Harold pia ametoa wito kwa Watanzania kutembelea duka hilo jipya la Sachsenküchen kujionea wenyewe bidhaa bora na kufurahia huduma hiyo mpya.
“Jikoni ni mahali ambapo mtu anatakiwa kufanya shughuli zake kwa furaha. Bidhaa zetu zimetengenezwa kuhakikisha matumizi mazuri ya nafasi huku pia zikiwa ni za kisasa, zenye kuvutia na kuridhisha wateja,” ameongeza Harold.
“Hapa Sachsenküchen kila kitu kinapewa kipaumbele, hususan ubora wa bidhaa ambazo zinabadilisha na kulifanya liwe ni sehemu halisi ya kuishi,” amesema.
Sachsenküchen ni kiwanda kipo Dippoldiswalde, karibu na Dresden, Ujerumani, na wamekuwa wakisanifu majiko na kutengeneza vifaa vya jikoni kwa zaidi ya miaka 100.
Tokea miaka ya 1990, Sachsenküchen imekuwa ikikua huku ikiwa na wafanyakazi 220 na inasavifirisha zaidi ya asilimia 50 ya bidhaa zake nje ya nchi, mapato ya Euro milioni 40 kwa mwaka huu faida ikiwa ni asilimia 12.
No comments:
Post a Comment