Foreign Exchange Rates

DStv Advert_090724

DStv Advert_090724

SBT Tanzania Advert_291123

Friday, 8 November 2019

BENKI YA NMB YATOA MISAADA ARUSHA, KILOLO, MUFINDI NA RORYA

Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Mrisho Gambo (kushoto) akisalimiana na mmoja wa wanafunzi wa Shule ya Sekondari Mrisho Gambo ya jijini Arusha wakati wa hafla ya kukabidhiwa meza na viti vyenye thamani ya shilingi milioni 10 vilivyotolewa na benki ya NMB. Katikati ni Meneja wa NMB Kanda ya Kaskazini, Aikansia Muro.
Wanafunzi wa shule ya Sekondari Kihaka wilayani Kilolo, Iringa wakiwa wamebeba stuli za maabara muda mfupi baada ya kukabidhiwa na benki ya NMB. Benki ya NMB ilikabidhi meza na stuli 60 vyote vikiwa na thamani ya shilingi Milioni 10.
Wanafunzi wa shule ya Msingi Maduma iliyoko Kata ya Maduma Wilayani Mufindi wakishangilia madawati waliyokabidhiwa na benki ya NMB juzi shuleni kwao.
Mkuu wa Wilaya ya Rorya, Simon Chacha akiwa ameketi na wanafunzi wa shule ya Msingi Minigo juzi (Jumanne) katika moja ya madawati yaliyotolewa na benki ya NMB ili kusadia kupunguza uhaba wa madawati shuleni hapo. Wengine ni Kaimu Meneja wa Kanda ya Ziwa (Mwenye koti na Tai Nyeusi), Amos Mubusi.

No comments:

Post a Comment