Foreign Exchange Rates

DStv Advert_090724

DStv Advert_090724

SBT Tanzania Advert_291123

Tuesday 8 October 2019

CEED TANZANIA YATOA MAFUNZO YA KUKUZA NA KUSIMAMIA BIASHARA KWA WAJASIRIAMALI NCHINI

Elizabeth Swai akizungumzia uzoefu wake wakati wa semina ya CEED Tanzania, jijini Dodoma hifi karibuni.
Archad Kato kutoka kampuni ya uzalishaji mvinyo ya Alko Vitanges amezungumzia fursa, uzoefu pamoja na changamoto mbalimbali katika ukuzaji wa biashara zao.
Dodoma - Kituo cha Ujasiriamali na Maendeleo ya Utendaji (CEED), yawakutanisha wajasiriamali mbalimbali jijini Dodoma katika semina iliyolenga kutoa elimu ya usimamizi na ukuzaji biashara zao ndani ya jiji la Dodoma.

Akizungumza na waandishi wa habari, mwakilishi kutoka CEED Tanzania, Fred Laiser amesema semina hii ni kwa ajili ya kuwapa ujuzi wa namna ya kuboresha biashara zao, ushindani wa kusaka fursa mbalimbali kutoka na kuongeza kwa idadi kubwa ya watu baada ya serikali kuhamishia shughuli zake hapa Dodoma.

"Sisi CEED Tanzania lengo letu kuu ni kuwasaidia wajasiriamali hapa nchini kukuza biashara zao. Leo tupo hapa Dodoma kwa lengo kuwapa elimu na kutoa fursa mbalimbali za kibiashara ambazo wajariamali wanaweza kuzichangamkia. Pia kuwakutanisha na wenzao wajifunze namna ya kukuza biashara zao, kutatua changamoto zao.’’ Alisema Bwana Laiser.

Mbali na hilo, Bwana Fred Laiser ametumia nafasi hii kuwataka wajasirimali mbalimbali nchini kujitokeza kwa wingi katika semina mbalimbali za ujasiriamali hasa zinazoendeshwa na CEED Tanzania kwaji ajili ya kupata ujuzi wa biashara zao na pia kufahamiana na wajasiriamali kutoka kila kona ya Tanzania.

Kwa upande wa wanufaikaji wa mafunzo haya, Bi.Elizabeth Swai mwanzilishi wa kampuni ya ufugaji kuku ya AKM Glitters Limited na Bwana Archad Kato kutoka kampuni ya uzalishaji mvinyo ya Alko Vitanges wamezungumzia fursa, uzoefu pamoja na changamoto mbalimbali katika ukuzaji wa biashara zao.

"Nawapongeza sana CEED Tanzania kwa kutupa nafasi hii ya kujifunza na kukutana na wajasiriamali wenzetu ili kujifunza mambo mbalimbali kutoka kwao. Moja ya changamoto inayotukabili sisi wajasiriamali hapa nchini ni kushindwa kuendeleza biashara zetu mara baada ya kuanzisha. Wengi tunapenda kujiajiri lakini wachache ndio wanaofikia malengo yao. Ili kutatua changamoto hizi, inatupasa kujifunza vitu vipya kila siku na kujaribu mara kwa mara mpaka pale biashara itakapoweza kujiendesha yenyewe", alisema Bwana Archad Kato.

Kwa upande wake, Elizabeth Swai ametumia nafasi hii kuwataka wajasiriamali kutumia vizuri teknolojia katika kujifunza masuala mbalimbali kwasababu teknolojia imerahisisha kila kitu kwasasa. Rahisi kupata taarifa mbalimbali zitakazowasaidia kujielimisha na kukuza biashara zao.

Semina hii imehudhuriwa na wajasiriamali takribani 52 kutoka kona mbalimbali za Dodoma na nje ya Dodoma ambapo kwa pamoja, wameweza kujadili masuala mbalimbali katika kukuza biashara zao, namna ya kutatua changamoto mbalimbali zinazowakabili katika shughuli zao za kila siku za ujasiriamali.

No comments:

Post a Comment