Meneja Bidhaa na Uwekezaji wa Benki ya NBC Bi Dorothea Mabonye (kulia) akizungumza wakati wa hafla ya uzinduzi wa kampeni hiyo. |
Kampeni hiyo ya miezi sita imetajwa kuwa inalenga kuwafikia maelfu ya watanzania ambao bado hawajafikiwa na huduma za kibenki kwa kuwa inahusisha namna rahisi zaidi ya kufungua akaunti hizo.
Akizungumza wakati wa warsha fupi ya Uzinduzi wa Kampeni hiyo iliyofanyika jijini Dar es Salaam hivi karibuni, Kaimu Mkurugenzi wateja wa Rejareja wa Benki ya NBC Bw Benjamin Nkaka alisema kampeni hiyo inalenga kuleta mabadiliko kwenye mtazamo wa uhifadhi wa akiba miongoni wa watanzania kutoka kuhifadhi pesa majumbani na badala yake wazihifadhi kupitia benki hiyo huku wakifurahia faida.
“Ni wakati muafaka sasa kwa watanzania mmoja mmoja au vikundi kuacha kuhifadhi fedha zao kwenye vibubu au namna nyingine yoyote ile majumbani mwao kwa kuwa njia hizo si salama kwao na kiuchumi pia na badala yake wanaweza kuhifadhi pesa zao kupitia akaunti ya Malengo ya NBC ambayo inawahakikishia usalama wa fedha zao huku pia wakifurahia faida zinazotolewa na benki’’ Alisema.
Alizitaja faida zitokanazo na akaunti hiyo ambazo mbali na kuokoa pesa za mteja, pia inaweza kubadilika kuwa amana kulingana na mapato ya mteja. Pia inatoa fursa kwa mteja kuweza kuweka akiba hiyo kupitia mashine za kuwekea fedha (ATM) za benki hiyo zinazopatikana kote nchini, kwenye matawi na kupitia mawakala wa huduka za benki hiyo.
“Habari njema zaidi ni kuwa hakutakuwa na makato ya mwezi huku pia mteja akipata riba ya hadi kufikia asilimia 7 kwa mwezi,’’ aliongeza.
Aidha Bw Nkaka alibainisha kuwa kampeni hiyo, inawalenga wateja wote wapya wa benki hiyo pamoja na wale ambao tayari wanamiliki Akaunti ya Malengo ya benki hiyo huku akisisitiza kuwa walengwa ni mtu mmoja mmoja na si kampuni au taasisi.
“Zaidi kupitia kampeni hii benki ya NBC inatoa faida mara mbili kwa wateja ambapo mteja atafurahia faida hizo zitokazo na Akaunti za Malengo huku pia akipata nafasi ya kushinda zawadi tofauti wakati wote wa kampeni hii,’’ alisema.
Alisema zawadi zitolewazo kwa mwezi zinahusisha kutoa ofa kwa mteja atayeweka kiasi cha sh 100/- kwenye akaunti ya Malengo kuweza kupata nafasi moja ya kuingia kwenyedroo ya mwezi.
"Hivyo hivyo pia kwa washindi wa kila mwezi ambapo jumla ya pikipiki tano (5) aina ya Yamaha zitatolewa kila mwezi ambapo hadi kufikia mwezi Disemba mwaka huu jumla ya piki 20 zitakuwa zimetolewa kwa washindi wetu,’’
“Sambamba na hilo pia kutakuwa na ofa ya safari iliyogharamiwa kila kitu kwenda Hifadhi ya Serengeti kwa ajili ya mapumziko ya mwisho wa mwaka kwa washindi watatu pamoja na wenza wao jumla wakiwa sita pamoja na safari kama hiyo kwenye Visiwa vya Seychelles kwa washindi watano na wenza wao ambao jumla watakuwa watu 10,’’ alifafanua.
Kwa upande wa zawadi Kuu Bw Nkaka alisema wateja ambao watakuwa na ongezeko la akiba la TZS 1,000,000/= katika kipindi cha kampeni hiyo watapata tiketi ya kuingia kwenye droo itayowapa nafasi ya kushinda pikipiki ya kubebea mizigo ya magurudumu matatu kwa washindi watatu.
"Kadri mteja anavyozidi kujiwekea akiba ndivyo anavyojiongezea nafasi ya kushinda kiasi cha sh TZS 500,000 na kupata uwekano mara tano zaidi wa yeye kushinda dhidi ya Yule atakayejiwekea akiba ya sh TZS 100,000 tu. Zawadi hizi zitasaidia wateja wetu kuongeza mapato yao au kuondokana na shida ya usafiri katika shughuli zao za kila siku,’’ aliongeza.
No comments:
Post a Comment