Foreign Exchange Rates

DStv Advert_090724

DStv Advert_090724

SBT Tanzania Advert_291123

Saturday, 21 September 2019

KAMPUNI YA VODACOM YALIPA ZAIDI YA TZS BILIONI 54.5 KAMA GAWIO KWA WANAHISA

Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Kampuni ya Vodacom Tanzania Plc, Bw. Ali Mufuruki (katikati) akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kumalizika kwa mkutano wa mwaka wa wanahisa wa Vodacom uliofanyika jijini Dar Es Salaam. Wengine pichani ni Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni hiyo Hisham Hendi (kushoto) na Mkurugenzi wa Fedha Jacques Marais.

Mkuu wa Mipango na Uwekezaji wa Vodacom Tanzania Plc, Hilda Bujiku akizungumza na wanahisa waliohudhuria mkutano mkuu wa mwaka wa wanahisa wa Vodacom Tanzania jijini Dar Es Salaam.
  • Vodacom yatoa taarifa ya ongezeko la faida kwa mwaka kufikia TZS billioni 90.2
Dar es salaam, 20 Septemba 2019 - Kampuni ya mawasiliano ya simu za mikononi inayoongoza Tanzania, Vodacom Tanzania PLC imetangaza faida ya mwisho wa mwaka ya kiasi cha TZS bilioni 90.2 kwa mwaka wa fedha 2018/2019 ulioishia mwezi Machi mwaka huu.

Wakati huo huo Kampuni ya Vodacom ambayo ina mtandao wenye kasi zaidi nchini inajivunia thamani iliyojitengenezea katika kipindi cha miaka ya hivi karibuni ikiwemo TZS bilioni 54.5 ambazo zimelipwa kama gawio kwa wanahisa.

Ongezeko hili limechangiwa na kuongezeka kwa mapato yatokanayo na huduma ambayo yanafikia TZS bilioni 1018.9, ambayo yamesababishwa na kukua na kuimarika kwa mapato yatokanayo na huduma za M-pesa, ununuzi wa Intaneti (Bando) na mapato yatokanayo na ujumbe wa simu. Kampuni ya Vodacom imepata wateja wapya wapatao milioni 1.2 katika mwaka huu wa fedha jambo ambalo linaongeza idadi yake ya wateja kufikia milioni 14.1.

Katika mwaka huu wa fedha kampuni ya Vodacom ilifanya uwekezaji mkubwa wa zaidi ya TZS bilioni 171.4 sawa na (asilimia 16.7% ya Mapato) katika kupanua mtandao wake, kuongeza maeneo yanayopata mtandao wa 4G katika miji mikubwa nchini, kuongeza uwezo na kuboresha mtandao kuweza kutoa huduma ya data ya kiwango cha juu kwa wateja.

Wakati huo Shilingi bilioni 59 zimewekezwa katika mishahara, mafunzo na maendeleo ya wafanyakazi wake wa kudumu wapatao 548 pamoja na kutoa ajira isiyo ya moja kwa moja kwa zaidi ya Watanzania 127,000.

Akiongea katika mkutano mkuu wa mwaka wa kampuni ya Vodacom leo, Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa kampuni ya Vodacom bwana Ali A. Mufuruki amesema, “Kampuni ya Vodacom vile vile inajivunia uwekezaji wake katika jamii ambao una thamani ya jumla ya shilingi trilioni 1.1, ambazo ni fedha zilizochangiwa katika uwezeshaji wa jamii kupitia kodi, ada za udhibiti katika kipindi cha miaka mitatu iliyopita ambapo malipo ya zaidi ya Shilingi trilioni 0.4 yalifanyika katika mwaka 2019 peke yake.”

“Ukuaji katika sekta ya mawasiliano imekuwa wa pole pole katika kipindi cha miaka ya hivi karibuni. Tukiwa kama watendaji muhimu katika sekta hii, tunajivunia kuwa chanya katika ukuaji wa sekta hii,” alihitimisha bwana Mfuruki.

Kuhusu Vodacom:


Vodacom Tanzania PLC ni watoa huduma ya mawasiliano ya simu za mkononi wanaoongoza wenye mtandao wa data wenye kasi zaidi nchini. Tunatoa huduma za mawsiliano kwa zaidi ya wateja milioni 14. Kampuni ya Vodacom Tanzania pamoja na kampuni zake tanzu ni sehemu ya Kundi la makampuni ya Vodacom (Vodacom Group) iliyosajiliwa Afrika Kusini ambayo kwa upande mwingine inamilikiwa na kundi la makampuni la Vodacom Plc la Uingereza. Kampuni ya Vodacom imesajiliwa katika soko la hisa la Dar es salaam (DSE) kwa namba ISIN: TZ1886102715 Stock name: VODA.

Kwa taarifa zaidi tafadhali tembelea tovuti yetu: www.vodacom.co.tz

No comments:

Post a Comment