Maafisa wa Benki ya NMB, Ally Ngingite (kushoto) na Isaac Mgwassa (kulia) wakibadilishana mawazo na Kamishna Msaidizi; Tathmini na Ufuatiliaji, Semiyono. |
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kilimanjaro, S.R. Handuni akifurahia jambo na Afisa wa Benki ya NMB, Amanda Feruzi. |
Ahadi hiyo imetolewa na Meneja Mwandamizi wa Wateja Binafsi na Kati wa NMB, Ally Ngingite, katika siku ya pili ya Kikao Kazi cha Maofisa Waandamizi wa Jeshi la Polisi Makao Makuu, Makamanda wa Mikoa na Vikosi, kinachofanyika katika Bwalo la Maofisa wa Polisi, Oysterbay, Dar es Salaam.
Kikao Kazi hicho kiliozinduliwa Septemba 24, 2019 na Inspekta Jenerali wa Polisi (IGP), Simon Sirro, kimefika ukomo Ijumaa Septemba 27, 2019 ambapo kwa siku nne maofisa hao wamejadili juu ya mafanikio, changamoto na mikakati ya Kamisheni katika Kuzuia, Kupambana na Kutanzua Uhalifu.
Kupitia Kikao Kazi hicho kilichofanyika chini ya Kaulimbiu: Umoja Wetu Ndiyo Nguvu Yetu, Tudumishe Usalama Katika Uchumi wa Viwanda, wadau wa Jeshi la Polisi wamealikwa kushiriki, ikiwemo NMB iliyotoa ahadi ya ushirikiano wa kudumu, sambamba na huduma bora kwa askari polisi nchini.
Ngingite aliwataka maofisa na makamanda hao kuwa mabalozi wema wa benki hiyo kwa askari walio chini yao kote nchini na kwamba wanapaswa kuifanya NMB kama mshirika wa kweli katika kujikweza kiuchumi kupitia mikopo na aina nyingine za uwezeshaji kutoka katika benki hiyo.
“Makamanda na maofisa wote mlioshiriki Kikao Kazi hiki, mkitoka hapa huku mnafikiria namna sahihi ya kuboresha maisha yenu ya sasa na baadaye, kukuza pato lenu kuelekea Uchumi wa Kati, maana yake ni kuwa askari wote nchini walioko chini yenu watafikia kufanya hivyo pia.
“Unafuu wa huduma zetu kwa Askari wa Jeshi la Polisi, majeshi mengine na Wafanyakazi wa Serikali, unatokana na ukweli kwamba tunatambua, kuthamini na kujali mchango wenu kwetu kama taasisi ya kifedha,” alisema Ngingite, ambaye alipokea maoni mbalimbali kutoka kwa makamanda hao.
Aliwaomba askari hao wanapoamua kukopa, kuhakikisha wanaitumia mikopo hiyo kwa usahihi, na kwamba siri ya mafanikio iko katika kufikiria kabla ya kukopa, kufanya uwekezaji mdogo baada ya kukopa ili kutanua pato lao na hatimaye kupunguza makali ya marejesho.
Akizindua Kikao Kazi hicho juzi, IGP Sirro aliwataka askari hao kuhakikisha wanajitoa kadri wawezavyo katika kulitumikia taifa na kwamba yeye anatamani kumaliza nafasi yake Jeshi likiwa na heshima, ambayo itapatikana kwa kila mmoja kuacha unafiki, kwani likichafuka, watachafuka wote.
No comments:
Post a Comment