Wakazi wa Bukoba mkoani Kagera, sasa wanaweza kupata huduma mbali mbali za mawasiliano kutoka kampuni ya Tigo kwenye duka jiipya, kubwa na la kisasa lililoboreshwa.
Huduma zitakazotolewa kwenye duka hilo jipya ni pamoja na kurudisha line iliyopotea/haribika,huduma ya Tigo pesa, intaneti, usajili mpya wa line za simu kwa kutumia alama za vidole, huuduma za kibiashara za Tigo pamoja na mauzo ya vifaa vya mawasiliano kama simu.
Akizungumza wakati wa uzinduzi wa duka hilo mjini Bukoba, Mkurugenzi wa Tigo Kanda ya Ziwa Uthmaan Madati alisema maboresha katika duka hilo jipya ni sehemu ya mkakati wa kampuni ya Tigo kuboresha huduma zinazotolewa kwa wateja wake katika maduka yake ya kuhudumia wateja.
“Duka hili lipo kati kati kati ya mji sehemu ambayo inafikika kiurahisi kwa wakazi wa hapa Bukoba na maeneo ya jirani. Tumeboresha muonekana wake na kuongeza nafasi ili kuweza kuwahudima wateja wengi zaidi na kuwafanya wateja wetu wafurahie huduma kila wanapofika hapa katika duka hili,” alisema Madati
Mgeni rasmi katika uzinduzi wa duka hilo Mkuu wa Mkoa wa Kagera Bregedia Generali Marco Elisha Gaguti alisema amefurahishwa na hatua iliyochukuliwa na kampuni ya Tigo kuboresha duka hilo na kufanya kuwa la kisasa na zaidi na hivyo kuweza kutoa huduma zenye ubora wa kimataifa.
“Huduma bora kwa wateja ni jambo muhimu sana kwa biashara yoyote ile kwa kuwa inamfanya mteja kujiona kuwa kampuni inayomhudumia inamjali na hivyo kujenga uzalendo na bidhaa au huduma zinazotolewa na kampuni husika.Nimefarijika kuona kuwa Tigo imewekeza kwenye eneo hili la huduma kwa wateja ambalo ni muhimu sana,” alisema.
Duka hilo jipya lina sehemu maalum inayoweza kutumiowa na wateja kujaribu huduma na bidhaa mbali mbali za Tigo kama vile simu za mkononi kabla hawajazinunua.
“Hii inawasaidia wateja wetu kuthibitisha ubora wa bidhaa zetu ambazo zinaendana na mahitaji yao kabla ya kuzinunua na kuzitumia,” aliongeza Madati
Duka hilo lilipo mtaa wa Sokoine mkabala na soko kuu la Bukoba, litakuwa na uwezo wa kuhudumia wateja 285,000.
No comments:
Post a Comment