Foreign Exchange Rates

DStv Advert_090724

DStv Advert_090724

SBT Tanzania Advert_291123

Wednesday 13 March 2019

PROF. KABUDI NA DKT. MAHIGA WAKABIDHIANA MAJENGO YA OFISI ZA WIZARA ZAO MTUMBA, DODOMA

Waziri wa Katiba na Sheria, Mhe. Dkt. Augustine Mahiga akimkabidhi Mhe. Prof. Palamagamba Kabudi, Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, mchoro wa jengo la Ofisi za Wizara ya Mambo ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki zinazojengwa kwenye Mji wa Serikali uliopo Mtumba, Dodoma. Makabidhiano hayo yalifanyika tarehe 12 Machi 2019. Baada ya kukabidhiwa Prof. Kabudi alipongeza jitihada za Wizara chini ya usimamizi wa Mhe. Dkt. Mahiga kwa hatua kubwa iliyofikiwa kwenye ujenzi huo.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Katiba na Sheria, Prof. Sifuni Mchome akitoa maelezo mafupi kwa Mhe. Prof. Palamagamba Kabudi, Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki na Mhe. Dkt. Augustine Mahiga, Waziri wa Katiba na Sheria walipofika kwenye ofisi za Wizara ya Katiba na Sheria zinazojengwa kwenye mji wa Serikali uliopo, Mtumba jijini Dodoma kwa ajili ya makabidhiano.
Mhe. Prof. Kabudi na Mhe. Dkt. Mahiga wakiwa kwenye moja ya chumba cha jengo la ofisi za Wizara zinazojengwa Mtumba. 
Mhe. Prof. Kabudi akisalimiana na mmoja wa Wakurugenzi wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa alipotembelea ofisi za Wizara zinazojengwa Mtumba.
Mhe. Prof. Kabudi akiongozana na Mhe. Dkt. Mahiga kuelekea kwenye jengo la Wizara, Mtumba.
Mhe. Prof. Kabudi akisaini kitabu cha wageni na kutoa maoni yake kuhusu maendeleao ya ujenzi wa ofisi hizo.
Muonekano wa jengo la ofisi za Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki linalojengwa kwenye mji wa Serikali uliopo Mtumba, Dodoma.
Bofya hapa kwa picha zaidi

No comments:

Post a Comment