Foreign Exchange Rates

DStv Advert_090724

DStv Advert_090724

SBT Tanzania Advert_291123

Friday, 22 February 2019

HALMASHAURI YA CHATO / SHIRIKA LA NYUMBA LA TAIFA (NHC) WAZINDUA RASMI MAUZO YA VIWANJA

Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Nyumba la Taifa (NHC), Dk. Maulidi Banyani (kati kati) akizungumza kutoa neno la shukurani katika uzinduzi huo kulia kwake ni Mkuu wa Mkuu wa Wilaya ya Chato Injinia Msafiri Mtemi Simioni na kushoto kwake ni Waziri wa Nishati na mbunge wa jimbo hilo, Dk. Medard Kalemani. 
Waziri wa Nishati na mbunge wa jimbo hilo, Dk. Medard Kalemani (kulia) akimshukuru Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Nyumba la Taifa, Dk. Maulidi Banyani (kushoto) kwa mchango wake katika upimaji wa viwanja hivyo vilivyozinduliwa mauzo.
Mkuu wa Wilaya ya Chato Injinia Msafiri Mtemi Simioni akizunguma katika uzinduzi huo kushoto kwake ni Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Nyumba la Taifa, Dk. Maulidi Banyani na Waziri wa Nishati na mbunge wa jimbo hilo, Dk. Medard Kalemani. Kulia kwake ni Mwenyekiti wa Halmashauri na Kaimu Mkurugenzi wa Wilaya hiyo, Philip Shoni.
Waziri wa Nishati na mbunge wa jimbo hilo, Dk. Medard Kalemani akizungumza katika hafla hiyo na kulia kwake ni Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Nyumba la Taifa, Dk. Maulidi Banyani.
Kaimu Mkurugenzi wa Hazina na Uendelezaji Biashara, William Genya (wa pili kulia) akijadiliana jambo na Meneja wa Wakala wa Majengo wa Serikali (TBA) mkoa wa Geita, Glagys Jeffta (wa kwanza kulia). Wanaoshuhudia kutoka kushoto ni Maafisa Uendelezaji Biashara, Clara Lumbanga, Phoibe Keu na Olivia Musanga Zoka. 
Eneo lililopimwa la Rubambangwe linavyoonekana kwa picha ya Drone,
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Chato, Eliud Mwaiteleke (kushoto) akijadiliana jambo na na Kaimu Mkurugenzi wa Masoko wa NHC, Itandula Gambalagi (katikati).
Hadhira ikifuatilia hafla hiyo ya uzinduzi.
TAARIFA KWA UMMA KUHUSU UUZAJI WA VIWANJA KATIKA ENEO LA RUBAMBANGWE HALMASHAURI YA WILAYA YA CHATO

Halmashauri ya Wilaya ya Chato ikishirikiana na Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) inautangazia umma juu ya uuzaji wa viwanja 1,035 vilivyopimwa na kuwekewa barabara katika eneo la Mlimani na Rubambangwe kata ya Muungano. Mauzo ya viwanja yanaanza wiki ijayo.

Wananchi wote mnakaribishwa kununua viwanja vyenye matumizi mbalimbali kama vile makazi, makazi na biashara, viwanja vya biashara, maeneo ya kumpumzikia, viwanja vya michezo na huduma mbalimbali za kijamii kama zahanati, Shule, Vituo vya Mafuta kwa bei ya kuanzia Tsh 1,300 kwa mita ya mraba.

Viwanja vipo mita chache kutoka katikati ya mji wa Chato. Vipo mkabala na barabara kuu iendayo Bukoba. Pembezoni mwa Ziwa Victoria.

Viwanja vilivyopimwa na kupangwa kwa ajili ya makazi vina ukubwa kama ifuatavyo;
  1. Ujazo wa juu (High density) 
  2. Ujazo wa kati (Medium density)
  3. Ujazo wa chini (Low density)  
Viwango vya gharama ya viwanja kwa matumizi mbalimbali;
  1. Makazi –Bei ya kiwanja kwa mita moja ya mraba ni Shilingi 1,300/=
  2. Makazi na biashara- Bei ya kiwanja kwa mita moja ya mraba ni Shilingi 1,700/=
  3. Biashara (Hotel, Vituo vya mafuta, maduka makubwa)- Bei ya kiwanja kwa mita moja ya mraba ni Shilingi 2,200/=
  4. Huduma za jamii (Zahanati, shule ya awali, sekondari) Bei ya kiwanja kwa mita moja ya mraba ni Shilingi 2,200/=
  5. Ibada/kuabudu- Bei ya kiwanja kwa mita moja ya mraba ni Shilingi 2,200/=
UTARATIBU WA KUNUNUA KIWANJA
  1. Chukua fomu ya maombi kutoka o­fisi za Halmashauri ya Wilaya ya Chato au Ofi­si ya NHC iliyo karibu nawe.
  2. Lipia angalau asilimia 30 ya thamani ya kiwanja unachonunua na kiasi kinachobaki kilipwe ndani ya siku 90.
  3. Malipo yote yafanyike kwenye akaunti ya benki ifuatayo: Jina la Akaunti: MRADI WA VIWANJA CHATO Nambari ya akaunti: 327 100 116 07 Benki: NMB Tawi la Chato
  4. Rejesha fomu ya maombi uliyojaza kwa usahihi ukiambatanisha pamoja na vielelezo vinavyohitajika ikiwemo nakala ya malipo (deposit slip) kutoka benki.
  5. Utapatiwa barua ya uthibitisho (Offer Letter) mara tu ombi lako litakapokubaliwa, pamoja na masharti ya kukamilisha malipo ya kiwanja unachochagua.
  6. Kwa maelezo zaidi tembelea ofisi za Idara ya ardhi ya Halmashauri ya Wilaya ya Chato.
Au KAMBARAGE House, 1 Mtaa wa Ufukoni, Dar es Salaam, Tanzania. Kwa Mawasiliano piga namba  +255 282 228 007/ +255 754 444 333.

No comments:

Post a Comment