Jengo la Makao Makuu ya Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA) likiwa limeanza kuinuka kuelekea ghorofa ya kwanza. |
Dk Mabula alitoa kauli hiyo jana tarehe 28 Januari 2019 wakati alipotembelea mradi wa ujenzi wa ofisi za Serikali katika mji wa Mtumba mkoani Dodoma unaojengwa na Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) ambalo liko chini ya Wizara yake.
Alisema kazi inayofanywa na shirika la Nyumba la Taifa kujenga ofisi za Serikali katika mji huo kwa sasa unaenda kwa kasi na unatia moyo kwani kila kukicha kila mhandisi anayesimamia mradi anakuwa anafanya ubinifu wake ambao ni tofaujti na wamwingine na hivyo kuchagiza maendeleo ya ujenzi wa majengo hayo.
Katika mradi huo Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) kupitia kampuni yake ya ujenzi inajenga ofisi za Wizara ya Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Wizara ya Fedha na Mipango, Wizara ya Nishati pamoja na Wizara ya Viwanda na Biashara.
Aidha, Dk Mabula amefurahishwa na ufuatialiaji wa ujenzi wa ofisi hizo unaofanywa na Wizara ya Fedha pamoja na Viwanda na Biashara na kueleza kuwa hatua hiyo inalifanya Shirika hilo kufanya kazi kulingana na mahitaji ya wateja wake.
No comments:
Post a Comment