Foreign Exchange Rates

DStv Advert_020324

DStv Advert_020324

SBT Tanzania Advert_291123

Wednesday 14 November 2018

TANZANIA KUPOKEA WATALII 10,000 KUTOKA SHANGHAI MWAKA 2019

Balozi wa Tanzania nchini China, Mhe. Mbelwa Kairuki akitoa neno la ukaribisho katika mkutano wa kutangaza vivutio vya utalii uliofanyika Shaghai, China tarehe 12 Novemba 2018.
Kutoka kushoto ni Mkurugenzi wa Bodi ya Utalii Tanzania, Bi. Devotha Mdachi, Balozi wa Tanzania nchini China, Mhe. Mbelwa Kairuki, Mwenyekiti wa Bodi ya Utalii Tanzania, Jaji Mstaafu, Thomas Mihayo na viongozi wa kampuni ya Touchroad International Group wakiwa katika furaha baada ya kukamilika uwekaji saini wa makubaliano ambapo kampuni hiyo italeta watalii 10,000 nchini Tanzania mwaka 2019.
Wajumbe wameshika shuka la kimasai ambalo linaonesha utamaduni wa kabila hilo maarufu kutoka Tanzania.
Bodi ya Utalii Tanzania (TTB) imesaini makubaliano na kampuni ya Touchroad International Group ya China kwa ajili ya kusafirisha watalii 10,000 kutoka jiji la Shanghai kutembelea Tanzania mwaka 2019 kwa kutumia ndege Maalum (chartered flights).

Makubaliano hayo yalisainiwa sambamba na mikutano ya kutangaza utalii katika soko la China- Tourism Roadshow katika miji mitano ya China iliyoanza katika jiji la Shanghai tarehe 12 Novemba 2018.

Mikutano hiyo ni matokeo ya jitihada za Ubalozi wa Tanzania nchini China kwa kushirikiana na TTB ambapo katika mkutano wa kwanza uliofunguliwa na Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii, Dkt. Aloyce Nzuki, washiriki mbalimbali zaidi ya 200 walijitokeza wakiwemo makampuni ya utalii (tour operators), mawakala wa usafirishaji (travel agents), mashirika ya ndege (airlines), na vyombo vya habari.

Katika mkutano huo, Mkurugenzi wa Bodi ya Utalii, Bi. Devotha Mdachi alitoa mada maalum kuhusu vivutio vya utalii vilivyopo nchini Tanzania pamoja na fursa za uwekezaji katika sekta ya utalii.

Aidha, makampuni ya utalii kutoka Tanzania yalipata fursa ya kuelezea packages zao za utalii mahsusi kwa soko la China.

Kadhalika, Shirika la Ndege la Tanzania lilitumia fursa hiyo kutangaza juu ya mpango wake wa kuanza safari za moja kwa moja kutoka Tanzania hadi China katika mji wa Guangzhou mwezi Februari 2019.

No comments:

Post a Comment