Katika mikutano tofauti iliyofanyika siku ya Jumanne, Jumatano na Alhamisi wiki iliyopita, Nsekela alimtembelea Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi nchini, Jenerali Venance Mabeyo, Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa nchini, Kamishna Diwani Athumani na Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Kuzuia na Kupambana na Dawa za Kulevya, Rogers Siang’a.
Pamoja na kufanya utambulisho rasmi kwa viongozi hao, Nsekela ambaye aliambatana na Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Benki hiyo, Ally Laay na Maofisa wengine, alitumia pia nafasi hiyo kuwaelezea viongozi hao juu mikakati yake ya kuipeleka mbele zaidi Benki ya CRDB na kuomba ushirikiano zaidi wa kibiashara kutoka kwa viongozi hao na taasisi wanazoziongoza.
Kwa upande wao viongozi hao waandamizi, pamoja na kumpongeza Nsekela kwa uteuzi huo mkubwa, walimuahidi kumpa ushirikiano na kumhakikishia kuwa wako tayari kuendelea kuwa wadau wakubwa wa Benki ya CRDB katika mikakati yake ya kibiashara.
Viongozi hao pia walipongeza sana jitahada za Benki ya CRDB katika kusaidia juhudi za Serikali ya awamu ya tano inayoongozwa na Rais Dkt. John Pombe Magufuli, zenye kulenga kuleta mapinduzi ya kiuchumi kwa kujenga Tanzania yenye uchumi wa Kati unaoshamirishwa na viwanda.
Picha ya pamoja. |
No comments:
Post a Comment