Foreign Exchange Rates

DStv Advert_090724

DStv Advert_090724

SBT Tanzania Advert_291123

Monday, 5 November 2018

MKURUGENZI MKUU MPYA WA SHIRIKA LA NYUMBA LA TAIFA DKT. MAULID BANYANI AWASILI NHC MAKAO MAKUU

Picha za matukio mbalimbali wakati Mkurugenzi Mkuu Mpya wa Shirika la Nyumba la Taifa (NHC), Dkt. Maulid Banyani alipowasili leo asubuhi katika makao makuu ya Shirika hilo. Pamoja na mambo mengine, Mkurugenzi Mkuu huyo alijitambulisha na kuwatambua Makaimu Wakurugenzi na Wakurugenzi wa NHC.

Mkurugenzi Mkuu mpya wa Shirika la Nyumba la Taifa (NHC), Dkt. Maulid Banyani akiwa katika ofisi yake Makao Makuu ya NHC.
Aliyekuwa Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Nyumba la Taifa (NHC),  Felix Maagi akimpokea Mkurugenzi Mkuu mpya Dkt. Maulid Banyani katika ofisi za Makao Makuu ya Shirika la Nyumba la Taifa asubuhi ya leo. 
Mkurugenzi Mkuu wa NHC akisalimiana na Kaimu Mkuu wa Kitengo Mawasiliano na Huduma kwa Jamii, Yahya Charahani.
Mkurugenzi Mkuu akikaribishwa na Afisa Mawasiliano wa Shirika la Nyumba la Taifa, Bi. Domina Rwemanyila.
Meneja Ofisi ya Mkurugenzi Mkuu, Arden Kitomari akisalimiana na Mkurugenzi Mkuu Dkt. Maulid Banyani wakati alipoingia rasmi katika Ofisi yake mpya.
Aliyekuwa Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Nyumba la Taifa, Felix Maagi akiwa na Mkurugenzi mpya wa NHC Dkt. Maulid Banyani.



Aliyekuwa Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Nyumba la Taifa,  Felix Maagi akimtambulisha Mkurugenzi Mkuu mpya Dkt. Maulid Banyani kwa Menejimenti ya Shirika. 
Kaimu Mkurugenzi wa Mauzo na Masoko,  Itandula Gambalagi akijitambulisha kwa Mkurugenzi Mkuu. 
Kaimu Mkurugenzi wa Hazina na Uendelezaji Biashara, William Genya akijitambulisha kwa Mkurugenzi Mkuu.
Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Nyumba la Taifa, Dkt. Maulid Banyani akisisitiza jambo kwa Menejimenti ya Shirika. 


Mkurugenzi Mkuu, Dkt. Maulid Banyani akiwa katika picha ya pamoja na Menejimenti ya Shirika la Nyumba la Taifa.


Mkurugenzi Mkuu Dk. Maulid Banyani akisaini kitabu cha wageni.

No comments:

Post a Comment