Foreign Exchange Rates

DStv Advert_090724

DStv Advert_090724

SBT Tanzania Advert_291123

Tuesday, 30 October 2018

UBELGIJI YAAMBIWA IONGEZE UWEKEZAJI NCHINI, MHANDISI MANYANYA

Naibu Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Mhe. Mhandisi Stella Manyanya akitoa hotuba ya ufunguzi kwenye kongamano la biashara kati ya Tanzania na Ubelgiji. kongamano hilo lilifanyika katika Hoteli ya Serena jini Dar Es Salaam.
Mkurugenzi wa Kukuza Uwekezaji kutoka Kituo cha Uwekezaji Tanzania, Bw. John Mathew Mnali akiongea katika kongamano hilo.
Wafanyabiashara kutoka Ubelgiji na Tanzania na wageni waalikwa wakimsikiliza Naibu Waziri wakati akitoa hotuba ya ufunguzi wa kongamano la biashara katika Hoteli ya Serena. 
Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Ulaya na Amerika kutoka Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Bw. Jestas Nyamanga (kulia) pamoja na wafanyabiashara kutoka Ubelgiji wakimsikiliza Mhe. Naibu Waziri Manyanya.
Ubelgiji imetakiwa kuongeza kiwango cha uwekezaji nchini ili kuchochea zaidi kasi ya azma ya Serikali ya awamu ya tano ya kuifanya Tanzania kuwa nchi ya viwanda na uchumi wa kati ifikapo mwaka 2025.

Kauli hiyo ilitolewa leo na Naibu Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Mhe. Mhandisi Stella Manyanya (Mb) alipokuwa anatoa hotuba ya ufunguzi wa Kongamano la Wafanyabiashara wa Ubelgiji na Tanzania linalofanyika katika Hoteli ya Serena jijini Dar Es Salaam.

“Kuna miradi 32 yenye thamanai ya Euro milioni 902 ambayo imeajiri wafanyakazi 1814 inayomilikiwa na wawekezaji kutoka Ubelgiji nchini Tanzania. Hivyo, kuna umuhimu wa kuongeza uwekezaji huo kwa kuwa mazingira ya uwekezaji nchini ni mazuri na yanavutia”, Mhandisi Manyanya alisema.

Mhe. Naibu Waziri aliwahamiza wawekezaji hao ambao ni wafanyabiashara wakubwa nchini Ubelgiji kuwekeza katika sekta za kilimo, hususan kwenye maeneo ya viwanda vya nguo, sukari, mafuta ya kupikia, maziwa, ngozi, nyama, mbegu, matunda na maua,

Sekta nyingine aliyoitaja ni ya nishati hasa katika miundombinu ya kuzalisha na kusambaza gesi asilia na nishati jadilifu.
Maeneo mengine yaliyosisitizwa na Mhe. Naibu Waziri ni pamoja na sekta ya utalii, madini, uvuvi katika bahari kuu, miundombinu, maeneo maalum ya viwanda (industrial parks) na ujenzi wa majengo hususan katika mji mkuu wa Dodoma ambapo mahitaji ni makubwa.

Uzalishaji wa dawa za binadamu na wanyama, vifaa tiba na uzalishaji wa samani za kisasa ni maeneo ambayo Mhe. Naibu Waziri aliwasihi wawekezaji hao kuyapa jicho la pekee.

No comments:

Post a Comment