Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa NHC, Félix Maagi akimkaribisha Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Temeke, Awadhi Haji kwenye eneo la tukio. |
Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Temeke, Awadhi Haji akisalimiana na wafanyakazi wa Shirika la Nyumba la Taifa. |
Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa NHC, Félix Maagi akimkabidhi hati ya makabidhiano ya kituo Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Temeke, Awadhi Haji. |
Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Temeke, Awadhi Haji akionyesha hati ya makabidhiano ya kituo mara baada ya kukabidhiwa hati hiyo na Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa NHC, Félix Maagi. |
Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Temeke, Awadhi Haji akikata utepe kama ishara ya kukabidiwa kituo hicho cha Polisi Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Temeke, Awadhi Haji. |
Ujenzi wa kituo hicho ni sehemu ya utekelezaji wa sera ya NHC ya huduma kwa jamii ambayo inaelekeza kurejesha sehemu ya kile kinachopatikana kwa jamii katika sehemu mbalimbali zilizokuwa na miradi na hata sehemu zingine ambapo miradi haifanyiki.
Akizungumza wakati wa ufunguzi na makabidhiano, Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa NHC, Felix Maagi amesema kuwa kabla ya ujenzi wa nyumba 208 za Shirika hilo katika eneo la Kibada, walipanga kujenga kituo hicho ambacho sasa kimeshakamilika ikiwa kuhakikisha wakazi wanaoishi katika nyumba hizo wanakuwa na ulinzi wao na mali zao.
Amesema kituo hicho chenye vyumba viwili vya mahabusu (wa kiume na wa kike), ofisi ya mkuu wa kituo, vyoo viwili vya maofisa na vya mahabusu.
"Kumekuwa na mawasiliano na Jeshi la Polisi kabla na wakati wa ujenzi na hivyo kukifanyia maboresho kituo hicho ambacho sasa kimekidhi viwango vya ubora vya mahitaji ya polisi na kitawahudumia wakazi wengi wa eneo hili, "amesema Maagi.
Naye Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Temeke, Awadhi Haji, alilishukuru shirika hilo kwa kuonesha uzalendo na kueleza kuwa, usalama ni muhimu kwa wananchi ili waweze kuishi kwa amani na kujiletea maendeleo.
"Sasa ni jukumu letu kukitunza kituo hiki na kuwalinda wananchi na mali zao. Hata hivyo kwa asilimia mia moja hatutaweza peke yetu bila wananchi kushirikiana nasi kufichua uhalifu na wahalifu, "alisema Kaimu Kamanda Haji.
Haji ambaye pia alimwakilisha Kamanda wa Kanda Maalum, Lazaro Mambosasa, amesema kituo hicho kwa sasa kitatoa huduma kwa saa 12 kutokana na kuwa ni kidogo na NHC wamekubali kukiongeza ili kiongeze huduma kwa kufanya masaa 24 na kuhimiza kuunda kikundi cha ulinzi shirikishi ili kushifikiana na polisi kuimarisha ulinzi zaidi.
Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa wa Changanyikeni, Gwalugano Mwakatobe, aliishukuru NHC na kuekeza kuwa, awali walilazimika kutembea zaidi ya kilomita tisa kufuata huduma na uwepo wa kituo hicho utaimarisha usalama na kuondoa ubambikizaji wa kesi kwa raia.
Aliyeteuliwa kuwa Mkuu wa Kituo hicho, Jacob Daqaro, aliwaomba wananchi ushirikiano na kuahidi kusimamia sheria, haki na usalama.
Kituo hicho kipo katika eneo lá mradi wa nyumba 208 za NHC Kibada, Kigamboni na Katibu wa Chama cha Wamiliki wa Nyumba hizo, Juvenal Jaka Mwambi, alishukuru Polisi kwa kuanza kazi jana mara baada ya makabidiano na kusisitiza ushirikiano.
No comments:
Post a Comment