Kampuni ya simu za mkononi ya Airtel imezindua mnara wa mawasiliano wenye uwezo wa kutoa huduma za Intanet kwa kiwango cha 3G kwa wakazi wa Kata ya Mikumi ikiwa ni hatua ya Kampuni hiyo kurahisha huduma za masafa ya Mtandao kwa wateja wake na watalii wanaotembelea katika hifadhi ya taifa ya Mikumi.
Akizindua Mnara huo wenye uwezo wa kutoa huduma za mtandao kwa masafa ya 3G Diwani wa kata ya Mikumi Rivinus Mwawira amesema, Mbali na upatikanaji wa Masafa ya Mtandao lakini pia wakazi wake zaidi ya elfu 30 watapata fursa mbalimbali za kimaendeleo kama kutuma na kupoke fedha kwa urahisi na pia huduma ya mawasiliano ya kawaida ya simu za mkononi.
“Mimi na wananchi wangu wa Mikumi tumekuwa na shauku kubwa ya kupata mnara huu, lakini jambo kubwa zaidi ni upatikanaji wa Masafa ya 3G kwani utaturahisishia sana kazi zetu kwani ukiwa na Internet ya uhakika kila kitu kinakua rahisi” Amesema bw Mwawira
“Manufaa Mengine yanayopatikana kutokana na uwepo wa Mnara huu hapa kwetu ni pamoja na wanafunzi kujisomea kwa kutumia program mbalimbali zinazopatikana mtandaoni ikiwa ni pamoja na Masomo ya Ufundi ya VSOMO inayotolewa kwa ushirikiano baina ya Airtel na VETA” Amesisitiza Diwani huyo
Kwa upande wake Meneja mauzo wa Airtel Kanda ya Morogoro Gibson Renatus alielezea kuwa manufaa yanayopatikana baada ya kuzinduliwa kwa mnara huo katika eneo la mikumi ni pamoja na upatikanaji wa mawasiliano ya simu za mkononi, Huduma ya Airtel Money na huduma bora za mtandao za 3G.
Baadhi ya Wananchi wa eneo la Mikumi wameelezea furaha yao baada ya kuboreshwa kwa mfumo wa mawasiliano wa kampuni ya Airtel katika eneo lao.
“Sasa hivi tunaweza kutuma na kupokea fedha kwa urahisi kupitia Airtel Money, tunapata internet yenye kasi ya 3G na pia hatupati tabu kupiga na kupokea simu tukiwa popote ndani nan je ya eneo letu la Mikumi” walieleza wananchi hao
Kuzinduliwa kwa mnara huo wenye uwezo wa kutoa huduma za mawasiliano na mfumo wa Internet wa 3G utawawezesha wakazi Zaidi ya elfu 30 wa kata ya mikumi na maeneo ya jirani kutuma na kupokea fedha, kuwa na mawasiliano ya uhakika wakati wote, kutumia internet kupakua na kupakia taarifa mbalimbali na hivyo kurahisha shughuli zao za kila siku.
No comments:
Post a Comment