Mhe. Waziri Mkuu akizungumza na Bw. Qiung mara baada ya kumkaribisha Ubalozini. |
Mhe. Waziri Mkuu akimtambulisha Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Augustine Mahiga kwa Naibu Meya Qiung wakati wa mazungumzo rasmi kati ya Waziri Mkuu na Naibu Meya. |
Naibu Meya Qiung (wa tatu kulia) akiwa na ujumbe aliofuatana nao wakimsikiliza Waziri Mkuu (hayupo pichani). |
Mazungumzo yakiendelea. Wa pili kulia ni Balozi wa Tanzania nchini China Mhe. Mbelwa Kairuki. |
Mhe. Majaliwa aliyasema hayo wakati wa mazugumzo yake na Naibu Meya wa Jimbo la Jiangsu nchini China, Bw. Guo Yuan Qiung aliyoyafanya tarehe 03 Septemba, 2018 katika Ubalozi wa Tanzania nchini humo ikiwa ni mwendelezo wa program yake ya kukutana na wadau muhimu wa maendeleo kabla ya kushiriki Mkutano wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa Jukwaa la Ushirikiano kati ya Afrika na China (FOCAC) utafanyika jijini Beijing kuanzia tarehe 01 hadi 04 Septemba, 2018.
Katika mazungumzo yao, Mhe. Waziri Mkuu alimweleza Naibu Meya huyo kuwa, Tanzania inaendelea kuboresha sekta ya kilimo kwa kushirikiana na wadau mbalimbali na kwamba jimbo la Jiangsu ni moja ya mdau muhimu ambaye anaweza kuchangia maendeleo ya Tanzania kwa kutumia teknolojia ya viwanda vya uchakataji mazao ili kuongeza thamani na kupata masoko ya uhakika kwa mazao hayo. Alisema kuwa kwa kuwa jimbo la Jiangsu ni miongoni mwa majimbo yaliyopiga hatua kubwa ya maendeleo ya teknolojia na viwanda duniani. Hivyo kushirikiana na Tanzania katika sekta za kilimo na viwanda kutaiwezesha nchi kufikia malengo yake ya kuwa nchi ya nchi ya viwanda ifikapo mwaka 2020 na nchi ya uchumi wa kati ifikapo mwaka 2025.
No comments:
Post a Comment