Kabla ya Mkutano huo ulioanza leo tarehe 19 Julai 2018 katika Hotel ya Windsor jijini Nairobi, Mheshimiwa Waziri Lukuvi alifanya ziara ya kikazi katika Wizara ya Ardhi na Upimaji nchini Kenya jana tarehe 18 Julai, 2018 ambapo pamoja na mambo mengine Waziri alitaka kujua mifumo ya upimaji, ugawaji, umiliki na utawala wa ardhi wa nchini Kenya. Maelezo ya mipango ya serikali ya nchi kuhusu ujenzi wa Nyumba pia yalitolewa.
Mambo mbalimbali yalijadiliwa katika mkutano huo ikiwa ni pamoja na kuondoa changamoto ya Rasilimali Fedha inayozikabili nchi nyingi za wanachama wa Umoja huo na kushindwa kuwapatia wananchi wa Afrika makazi bora na nafuu.
Kwa ujumla changamoto za nchi za kiafrika katika kuwapatia wananchi wa kawaida makazi nafuu zinafanana na kilio kikubwa katika nchi wanachama, ambazo ni kuwepo makazi holela hata baada ya nchi hizo kujikomboa kutoka ukoloni mkongwe.
Tanzania ni nchi mojawapo mwanachama wa Shelter Afrique kati ya nchi 44 za barani Afrika ilijiunga na Shelter Afrique mwaka 2003 na Mkutano wa 32 ambao ulifanyika N’djamena, Chad 2013, uliopitishwa na Azimio Namba GM/ 2013/005 la kuongeza Hisa kwa kila nchi mwanachama kwa lengo la kukuza mtaji wa Kampuni hiyo na kuiwezesha kuweka nguvu zaidi katika masuala ya uendelezaji nyumba barani Afrika.
Ujumbe wa Tanzania kwenye Mkutano wa 37 wa Makazi Afrika (Shelter Afrique) ukifuatilia mkutano huo wa leo. |
Waziri wa Ardhi Nyumba na Mendeleo ya Makazi Mheshimiwa William Vangimembe Lukuvi akijadiliana jambo na Katibu Mkuu wa Wizara ya Ardhi nchini Kenya jana. |
Waziri wa Ardhi na Upimaji wa Kenya, Mama Farida Karoney akijadiliana jambo na Waziri Lukuvi kwenye makao makuu ya wizara hiyo nchini Kenya. |
No comments:
Post a Comment