Foreign Exchange Rates

DStv Advert_090724

DStv Advert_090724

SBT Tanzania Advert_291123

Tuesday, 24 July 2018

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI KUHUSU ZIARA YA MHE. MKAPA NCHINI MSUMBIJI

Maadhimisho ya Miaka 50 ya Mkutano wa Pili wa Chama Tawala cha Msumbiji FRELIMO yatafanyika katika Jimbo la Niassa nchini Msumbiji tarehe 25 Julai 2018. Rais wa Jamhuri ya Msumbiji, Mhe. Filipe Nyusi alimwalika Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM), Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli kushiriki maadhimisho hayo. Kutokana na majukumu mengine ya kitaifa Mhe. Rais Magufuli hatoweza kushiriki. Hivyo, kwa kuona umuhimu wa mahusiano kati ya Tanzania na Msumbiji na umuhimu wa maadhimisho hayo kwa historia ya nchi hizi mbili, amemteua Rais Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Benjamin William Mkapa amwakilishe kwenye sherehe hizo na ataambatana na Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (Bara), Mhe. Philip Mangula.

Mahusiano kati ya Tanzania na Msumbiji
Mahusiano kati ya Tanzania na Msumbiji ni mazuri na yamekuwa yakiimarika kila wakati. Mahusiano kati ya nchi hizi yalianza enzi za harakati za ukombozi dhidi ya ukoloni wa Kireno nchini Msumbiji. Mahusiano hayo yalijengwa na waanzilishi wa mataifa haya mawili, Hayati Mwalimu Julius Kambarage Nyerere na Hayati Samora Moises Machel na yameendelea kuwa mazuri siku hadi siku na kuendelezwa na Viongozi wote Wakuu waliofuata wa nchi hizi mbili. Ziara za Viongozi wa ngazi mbalimbali wa Serikali na vyama tawala vya Chama Cha Mapinduzi (CCM) na FRELIMO wameendelea kutembeleana na kudumisha uhusiano huo.

No comments:

Post a Comment