Foreign Exchange Rates

DStv Advert_090724

DStv Advert_090724

SBT Tanzania Advert_291123

Tuesday, 17 July 2018

RAIS DKT. JOHN POMBE MAGUFULI AWEKA JIWE LA MSINGI CHUO CHA UONGOZI CHA MWALIMU JULIUS NYERERE KINACHOJENGWA KIBAHA KWA MFIPA MKOANI PWANI NA KUZUNGUMZA NA WANANCHI WA MAILIMOJA NA MBEZI. JULAI 16, 2018

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambaye pia ni Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na mgeni wake Waziri wa uhusiano wa Kimataifa wa Chama cha Kikomunisti cha China (CPC) Song Tao wanne kutoka kushoto pamoja na Makatibu wa vyama vya, CCM, ANC, SWAPO, ZANU-PF, MPLA, FRELIMO, wakiweka mchanga kama ishara ya uwekaji wa Jiwe la msingi Ujenzi wa Chuo cha Mwalimu Julius Nyerere kinachojengwa katika eneo la Kibaha kwa mfipa mkoani Pwani. Julai 16, 2018. 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambaye pia ni Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika picha na mgeni wake Waziri wa uhusiano wa Kimataifa wa Chama cha Kikomunisti cha China (CPC) Song Tao wanne kutoka kushoto waliokaa, viongozi wa vyama vya ANC, SWAPO,ZANU-PF, MPLA, FRELIMO pamoja na viongozi mbalimbali wa Chama cha Mapinduzi CCM mara baada ya kuweka jiwe la msingi ujenzi wa Chuo cha Uongozi cha Mwalimu Julius Nyerere kinachojengwa katika eneo la Kibaha kwa mfipa mkoani Pwani. Chuo hicho kinajengwa na Chama cha Kikomunisti cha China (CPC) kwa gharama ya Shilingi Bilioni mia moja(100).
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambaye pia ni Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza jambo na mgeni wake Waziri wa uhusiano wa Kimataifa wa Chama cha Kikomunisti cha China (CPC) Song Tao kabla ya tukio la uwekaji jiwe la msingi ujenzi wa Chuo cha Uongozi cha Mwalimu Julius Nyerere kinachojengwa katika eneo la Kibaha kwa mfipa mkoani Pwani.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambaye pia ni Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Dkt. John Pombe Magufuli akipiga ngoma pamoja Sophia Shaningwa Katibu wa Chama cha SWAPO kutoka nchini Namibia huku Waziri wa uhusiano wa Kimataifa wa Chama cha Kikomunisti cha China (CPC) Song Tao akipiga makofi mara baada ya uwekaji wa jiwe la msingi ujenzi wa Chuo cha Uongozi cha Mwalimu Julius Nyerere kinachojengwa katika eneo la Kibaha kwa mfipa mkoani Pwani.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambaye pia ni Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na wananchi kabla ya ya kuweka jiwe la msingi ujenzi wa Chuo cha Uongozi cha Mwalimu Julius Nyerere kinachojengwa katika eneo la Kibaha kwa mfipa mkoani Pwani.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na mamia ya wananchi wa Mbezi Mwisho waliosimama katikati barabara ya Morogoro kuhusu kero zao mbalimbali wakati akitokea Kibaha Kwa mfipa mkoani Pwani ambapo aliweka jiwe la Msingi ujenzi wa Chuo cha Uongozi cha Mwalimu Julius Nyerere. Julai 16, 2018. 

Bofya hapa kwa picha zaidi

No comments:

Post a Comment