Kampuni ya simu za mkononi ya Airtel inayoongoza kwa kutoa huduma bora za Smartphone kupitia kitengo chake cha rasilimali watu wameandaa bonanza la michezo lililowashirikisha wafanyakazi wake wote kwa lengo la kujenga afya za wafanyakazi hao pamoja na kuongeza ushirikiano eneo la kazi.
Akiongea mara baada ya tamasha hilo kuisha Mkuu wa kitengo cha Rasilimali Watu alisema “Airtel tunatambua jitihada za serikali zinazosisitiza kuboresha na kuweka mzingira rafiki sehemu za kazi, pia Airtel tunafahamu sana umuhimu wa michezo na mazoezi kwa afya za wafanyakazi wetu, Hivyo ndio maana tumeona ni vyema kukutana kwa michezo kama hivi ili kuwasaidia wafanyakazi kurelax na kubadilishana mawazo wakiwa katika mazingira tofauti”
Katika Bonaza hilo la muziki na mchezo wafanyakazi wengi walifurahia zaidi mchezo wa kupigiana penati ambao washiriki walikuwa ni wasichana wote kwa mgawanyo wa vitengo vyao vya kazi kikiwemo kitengo cha ofisi ya Mkurugenzi mkuu kinachoundwa na rasilimali watu na udhibiti huduma, kitengo cha masoko, huduma kwa wateja, kitengo cha mauzo, ununuzi na ugavi, pamoja na kitengo fedha na mipango.
Katika mchezo huo ushiriki ulikuwa wenye uvutano mkubwa kwa mzunguko wa ngazi ya mtoano na kuwa wenye ushindani mkali zaidi pale ambapo walibaki vinara watatu ambao ni kitengo cha Huduma kwa wateja waliokichapa kitengo cha fedha na mipango kwa goli 6 huku wao wakiambuia goli tano na kuwafanya kitengo cha huduma kwa wateja kuibuka washindi wa ujumla na kubeba kombe la ushindi wa mchezo huo.
Kibacha alisema “Airtel kupitia ofisi ya Rasilimali watu bado wataendelea na programu nyingine nyingi za kuwajenga na kuwaweka watoa huduma na wateja kuwa karibu zaidi”.
Kwa upande wake mkurugenzi mtendaji wa Aitel Bw Sunil Colaso aliwapongeza washindi wa Bonanza hilo na kuwataka wafanyakazi wake kuzingatia sana umakini pale wanapohudumia wateja.
“Niliona mwanzo mlianza kushindania kawaida mno lakini baada ya ushindani kupamba moto wote mkawa makini na mkawa mnalenga kwelikweli mpira usieme nje, sasa mnapaswa umakini huo pia muuzingatie kwenye kutoa huduma kwa wateja wetu wote tunapaswa kuwa makini hivi hivi” alisisitiza Colaso
Mkurugenzi huyo pia alisema kwa kuwa Airtel inashirikiana na wadau wengi watahakikisha hawaishii hapo wanawakutanisha na watoa huduma ili wafurahie kuwa ndani ya familia ya Airtel.
Tutakutana na wadau watoa huduma mbalimbali wiki ijayo ikiwa lengo ni kuwasaidianaupatikanaji wa huduma mbalimbali ikiwemo afya ya kinywa na macho, kujua jinsi yakujipatia bidhaa bora za vifaa vya moto kama magari, jinsi ya kupata mikopo ya Nyumba, viwanja na hata jinsi ya kuweka insuarance kwenye baadhi ya mali zao” alisema Colaso.
No comments:
Post a Comment