Foreign Exchange Rates

DStv Advert_090724

DStv Advert_090724

SBT Tanzania Advert_291123

Monday, 19 March 2018

BAADA YA KAULI YA RAIS JOHN MAGUFULI, WAFANYABIASHARA WAELEZA KERO ZINAZOWAKABILI TRA


Dar es Salaam. Siku chache baada ya Rais John Magufuli kuagiza kufuatiliwa namna ya utozaji wa kodi unaofanywa na Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), wafanyabiashara wameeleza kero mbalimbali wanazokabilianazo kutoka kwa maofisa wa mamlaka hiyo.

Baadhi ya kero hizo ni makadirio ya kodi kubwa tofauti na biashara au kipato wanachokipata, ushirikiano mdogo kati ya wafanyabiashara na TRA kuvizia wateja wanapotoka katika maduka mbalimbali.

Machi 14, Rais John, alimuagiza waziri wa fedha na mipango kufuatilia utozaji wa kodi unaofanywa na TRA ili kuepusha utozaji wa viwango ambavyo ni kero huku akisisitiza, “Inatakiwa kulipa kodi isiwe kero, iwe heshima.”

Akizungumza jana Frank Mboya alisema maofisa wa TRA, wamekuwa na mtindo wa kuwakadiria kodi kubwa tofauti na biashara wanayoifanya kwa kigezo kuwa tu wapo katikati ya jiji.

“Jambo hili linatuumiza sana wafanyabiashara wenye kipato cha chini kwa sababu tunalipa kodi kodi tofauti na kipato tunachokipata kwa mwezi. Lakini TRA tukiwaeleza hawatuelewi wanahisi tunakwepa kodi, hatuna nia hiyo kwa sababu lazima tulipe kwa sababu ipo kisheria kwa maendeleo ya nchi,”

Ashok Dewji aliungana na Mboya akisema suala la makaridio ya kodi ndiyo kero kubwa kwa wafanyabiashara wengi wa bidhaa mbalimbali kwa sababu TRA haiangalii ukubwa au udogo wa biashara, bali kodi.

“Mambo yakiendelea hivi nafikiria kufunga biashara yangu hii kwa sababu hakuna ninachokipata ukizingatia nina familia inayohitaji msaada wangu, lakini mwisho wa siku fedha zote zinaishia TRA,” alisema.

Mfanyabiashara huyo wa nguo alidai kuwa TRA wamekuwa na kawaida ya kuvizia wateja wao nje ya maduka na pindi wanapotoka na kuwaona wana kifurushi huwadaka na kuwadai risiti za malipo.

“Hiki siyo kitendo kizuri ni kero kwa wateja na wafanyabiashara kwa sababu tunaonekana siyo waaminifu. Tunamshukuru Rais Magufuli kwa kuliona hili,” alisema.

Katibu wa Jumuiya ya Wafanyabiashara Tanzania (JWT), Abdallah Mwinyi alimpongeza Rais Magufuli kwa kutoa kauli hiyo na akisema wanaomba utekelezaji wake uwe endelevu kwa sababu wafanyabiashara wana kero kubwa dhidi ya TRA.

Alisema suluhisho pekee la kuondokana na sintofahamu hizo zinazowakumbuka wafanyabiashara ni Rais Magufuli kuimarisha mfumo wa sheria wa ulipaji kodi.

Alisema maofisa wa ngazi za juu wa TRA tatizo lakini shida inakuja kwa wale wanaokwenda eneo la tukio.

“Tunamuomba Rais Magufuli atusaidiae mambo mawili ili kuondoa hali hii. Moja aandae mkakati wa kukutana wafanyabiashara hasa waagizaji ili kujadili changamoto wanazokumbana nazo katika utekelezaji wa msingi wa sheria ya ulipaji kodi.

Jambo jingine aunde tume kushughulika changamoto zinazohusiana na sheria ya ulipaji kodi ili hatua stahiki zichukuliwe.

Mwananchi

No comments:

Post a Comment