Foreign Exchange Rates

DStv Advert_090724

DStv Advert_090724

SBT Tanzania Advert_291123

Thursday, 8 February 2018

WAZIRI MAHIGA AHITIMISHA ZIARA NCHINI KOREA KUSINI

Mheshimiwa Dkt. Augustine Mahiga, Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki akiwa kwenye mazungumzo na Bw. Chang Yaong Hun, Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Exim ya Korea Kusini. Viongozi hao wawili walikutana kwenye ofisi za Benki hiyo Jijini Seoul Korea Kusini wakati wa ziara ya kikazi ya siku tatu ya Waziri Mahiga nchini humo.
4 Feb. 2018 - Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Dkt. Augustine Mahiga ameahidi kusimamia uimarishwaji wa uhusiano wa kiuchumi na biashara kati ya Tanzania na Korea Kusini ili wananchi wa pande zote mbili wapate manufaa. 

Waziri Mahiga ameyasema hayo alipokuwa anahitimisha ziara yake ya kikazi ya siku tatu ambapo siku ya mwisho aliitumia kikamilifu kukutana na taasisi za umma za biashara na viwanda, Benki ya Exim ya Korea pamoja na makampuni binafsi yanayojipanga kutekeleza miradi mbalimbali ya maendeleo nchini Tanzania. 

Amesema kuwa miaka 25 ya kwanza ya uhusiano wetu na Jamhuri ya Korea ilijikita kwenye kuweka misingi imara ya uhusiano wa kidiplomasia ambapo nchi zetu zilikuwa zinajiimarisha kama mataifa huru. “Sasa ni wakati wa kushamiri kiuchumi tuone sekta binafsi zinavyoshiriki katika kukuza uchumi, wananchi wa Tanzania waje kwa wingi nchini Korea kujifunza masuala ya teknolojia, uhandisi na hata usanifu na ubunifu. Huu ndio uhusiano wenye tija kwa mataifa yetu”. Mheshimiwa Waziri alisema.

Akizungumza na Bw. Chang Yaong Hun, Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Exim ya Korea, Mheshimiwa Mahiga mbali na kuishukuru taasisi hiyo kwa kuendelea kutoa mikopo na misaada nchini Tanzania, Waziri Mahiga alieleza kuwa Serikali ya Awamu ya Tano ya Mheshimiwa John Pombe Magufuli sasa imejikita kwenye mapambano dhidi ya rushwa na ujenzi wa viwanda ili kuleta maendeleo ya kweli kwa wananchi wetu. Kwasasa Benki hiyo inatekeleza miradi ya ujenzi wa miundombinu ya umeme na maji mikoa mbalimbali ya Tanzania ukiwemo Mkoa wa Dar es Salaam. 

Mheshimiwa Mahiga alifafanua kuwa ajenda ya Mheshimiwa Magufuli ya viwanda, haiwezi kukamilika bila kuwa na miundombinu ya msingi kama vile uzalishaji wa umeme wa kutosha na ukuaji wa sekta ya uchukuzi na mawasiliano ambapo Korea Kusini ni wabobezi kwenye masuala hayo. 

Alitumia fursa hiyo kumkaribisha Bw. Chang na timu yake kwenda Tanzania kufanya tathmini ya miradi tunayoshirikiana nao, lakini pia miradi mipya kwenye sekta ya uchukuzi kama ujenzi wa Standard Railway Gauge “SRG” kutoka Isaka hadi Kigali, n.k. ambayo ni miradi ya kipaumbele kwa sasa kwa taifa letu.

No comments:

Post a Comment