24
JANUARI 2018, Dar es Salaam – Mwalimu
Commercial Bank PLC (MCB) imezindua bidhaa iitwayo MCB Salary Advance, ikiwa
ni moja ya mkakati wake katika kuboresha maisha ya Watanzania kwa ujumla.
Akizungumzia
Kuhusu bidhaa hii mpya ya mkopo wa ‘MCB
Salary Advance’, Mkuu wa kitengo cha ukuzaji biashara na masoko, Bwana Valence
Luteganya alisema, mteja ataweza kuchukua mkopo huu pale anapouhitaji, Nia ni kuwezesha
mteja wetu kuyakabili mahitaji ya dharura yanayojitokeza wakati wowote.
Alisema, bidhaa ya salary advance
inayowalenga wateja wafanyakazi wanaopitishia mishahara yao katika Benki ya
Mwalimu, “Mkopo huu unariba nafuu na unapatikana
kwa urahisi na haraka, Lengo ni kutoa mkopo wa bei nafuu utakao wasaidia
wateja wetu kupunguza ukali wa Maisha”.
Aliongeza “Kupitia huduma ya Salary advance mfanyakazi
anayepitisha mshahara MCB, ataweza kupata hadi asilimia 50 ya mshahara wake kwa
riba nafuu. Kupata huduma hii mteja
anatakiwa kutembelea tawi la benki au
kutuma meseji kupitia whatsapp kwa kuandika neno ‘mshahara wangu’ kwenda namba 0629331755.
Naye
Mkuu wa kitengo cha huduma kwa njia ya mitandao Ndg. John Mhina aliongeza kwa
kusema “Huu ni mwendelezo wa mchakato maalum kuhakikisha tunatimiza mahitaji ya
wateja wetu mwaka 2018, na ni ishara
kuwa Benki ya Mwalimu imejipanga vyema katika kutoa bidhaa na huduma
zinazolenga maslahi ya watanzania hivyo kuufanya mwaka huu kuwa wa neema kwa
wateja wetu. Tunakaribisha Watanzania wote kuja kufungua akaunti na kuweza
kufaidi huduma na bidhaa zetu.
Kwa
taarifa zaidi wasiliana kwa:
Mwalimu
Commercial Bank Plc (MCB).
Mlimani
Tower - Mezzanine Floor, Sam Nujoma Road
P.O.
Box 61002, Dar es Salaam
Telephone:
022-2772954/7 and +255 629 331 151
Email; info@mcb.co.tz
No comments:
Post a Comment