Dar es Salaam, Januari 29, 2018 – Benki ya NMB (NMB Bank PLC) imepata faida baada ya kodi ya shilingi Bilioni 95 mwaka 2017.
Kutokana na changamoto za kibiashara zilizojitokeza mwaka 2017, Benki ya NMB iliweza kuongeza pato lililotokana na biashara ya benki kwa asilimia 5 kutoka shilingi bilioni 614 mwaka 2016 mpaka bilioni 647 mwaka 2017, Biashara ya benki iliendelea kuwa imara kipindi hiki. Kwa miaka mitano mfurulizo, benki ilitajwa kama benki bora nchini na kwa mara ya kwanza, ilitajwa kuwa benki bora inayoendelea barani Afrika na taasisi ya kiamataifa ya Euromoney.
Benki ya NMB ilipata faida baada ya kodi ya shilingi Bilioni 95 kwa mwaka 2017 chini ya shilingi Bilioni 154 iliyofikiwa mwaka 2016. Kushuka kwa faida hiyo kunatokana na ongezeko la changamoto za urejeshwaji wa mikopo kutoka kwa Wateja.
Kiwango kikubwa cha riba kilikuwepo mwanzoni mwa mwaka 2017. Hii ilitokana na ongezeko la asilimia 18 ya gharama za riba kutoka shilingi Bilioni 102 ya mwaka 2016 mpaka shilingi bilioni 120 ya mwaka 2017. Wakati huo huo mapato ya riba yaliongezeka kwa asilimia 4 kutoka shilingi Bilioni 449 kwa mwaka 2016 mpaka shilingi bilioni 467 kwa mwaka 2017.
Mapato ya biashara ya fedha za kigeni ilikuwa kwa asilimia 15 kutoka shilingi Bilioni 15 mwaka 2016 mpaka shilingi bilioni 18 mwaka 2017. Ada na kamisheni zilikua kwa asilimia 11 hasa kutokana na kuongezeka kwa miamala kutoka njia mbalimbali za kibenki; Pato lisilokuwa na riba (non-interest revenue) liliongezeka kwa asilimia 9 mpaka shilingi Bilioni 180.
Katika robo ya nne ya mwaka 2017, Amana za wateja nazo ziliongezeka kwa asilimia 9 hadi kufikia kiasi cha shilingi trilioni 4.2 robo ya nne ya 2017. Matokeo haya yaliifanya benki kukuza kitabu cha mikopo na hivyo mikopo ilikua mpaka kufikia shilingi bilioni 2,786 kwa robo ya tatu ya mwaka mpaka kufikia shilingi bilioni 2,787 katika robo ya nne ya mwaka 2017.
Wafanyakazi wa serikali waliobainika kuwa na vyeti feki na kuachishwa kazi na waajiri wao serikali katika robo ya kwanza ya mwaka 2017, ambapo baadhi yao walikuwa na mikopo ya NMB Bank na baadhi ya Wateja wakubwa walioshindwa kulipa mikopo yao kama ilivyotarajiwa ilisababisha kuongezeka kwa mikopo isiyolipika.
Benki ya NMB ipo kwenye mazungumzo na serikali na ina Imani kubwa kuwa kutakuwa na maamuzi ambayo yatasaidia kupunguza athari za mikopo, punguza mikopo isiyolipika na hivyo kuongeza faida ya benki.
Katika wakati ambapo biashara inalazimika kufanya marekebisho ili kuendana na mabadiriko ya mazingira ya ufanyaji biashara, benki ilichukua hatua mbalimbali ili kukabiliana na mikopo mibaya. Ikiwa ni pamoja na kupunguza baadhi ya huduma na pia kufuta mikopo isiyolipika kwenye vitabu vya mikopo ambayo imeweza kurekebisha Kiwango cha mikopo isyolipika (Non-Performing Loans) kutoka asilimia 9.3 ya robo ya tatu mpaka asilimia 6.4 kwa Desemba 31, 2017.
Mkurugenzi wa NMB Bank – Ms Ineke Bussemaker aliwahakikishia Wateja na wadau kuwa benki ipo imara na itaendelea na malengo yake ya kutoa huduma bora ya kifedha kwa watanzania wote. Mwaka 2017, benki ilifungua matawi mapya 23, vituo 10 vya kukusanya fedha na mawakala 2,389.
Katika utekelezaji wa IFRS 9, kuanzia Januari 1, 2018, Bi Bussemaker aliwahakikishia kuwa benki ina mtaji imara ambayo itaeendelea kuwa juu ya wastani uliowekwa na mamlaka za usimamiaji mabenki nchini. NMB Bank ilimaliza mwaka na uwiano wa utosherevu wa mtaji halisi wa benki wa asilimia 17 ukilinganisha na asilimia 14.5 inayotakiwa na Uwiano wa ukwasi wa benki (Liquid Asset Ratio) wa asilimia 39 ukilinganisha na Kiwango kinachohitajika cha asilimia 20.
Kwa Mawasiliano:
Joseline Kamuhanda, Maneja Mwandamizi kitengo cha Uhusiano
Email: Joseline.Kamuhanda@nmbtz.com
Anna Mwasha, Kaimu Mkuu wa Kitengo cha Mkakati na Mahusiano ya Wawekezaji
Email: Anna.mwasha@nmbtz.com
Kuhusu NMB:
NMB ni benki inayoongoza nchini Tanzania kwa matawi, ikiwa na zaidi ya matawi 213, wateja zaidi ya milioni 3 na zaidi ya mashine 700 za kutolea fedha (ATM) nchi nzima. NMB imeasisi ubunifu mkubwa katika soko la Tanzania ikiwa ni pamoja na huduma za benki kwa njia ya simu yaani NMB mobile , Pesa Fasta na malipo kwa kutumia mashine za ATM. NMB inaendelea kujikita katika kutoa huduma kwa makampuni makubwa, masoko ya kifedha pamoja na huduma za kusaidia makusanyo ya kifedha na biashara. Lakini Pia imekuwa mstari wa mbele katika maendeleo ya kilimo na imeanzisha mfumo wa stakabadhi ghalani kupitia vyama vya ushirika nchini.
Kwa Maelezo zaidi kuhusu NMB Bank, tembelea tovuti ya: www.nmbbank.co.tz
No comments:
Post a Comment