Foreign Exchange Rates

DStv Advert_090724

DStv Advert_090724

SBT Tanzania Advert_291123

Thursday, 14 December 2017

RAIS JOHN MAGUFULI AFUNGUA RASMI NYUMBA 150 ZA MAKAZI ZA SHIRIKA LA NYUMBA LA TAIFA (NHC) IYUMBU, DODOMA

Picha za matukio mbalimbali wakati Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. John Pombe Magufuli alipofungua mradi wa Nyumba za Gharama nafuu Iyumbu Satellite Centre jana. Mradi huu una jumla ya nyumba 150 kwa awamu ya kwanza na zitafuata nyumba zingine 150 katika awamu inayofuata.

Rais Dk. John Pombe Magufuli akifungua mradi wa Iyumbu Satellite Centre. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk John Pombe Magufuli amefungua mradi wa Nyumba za Gharama nafuu Iyumbu Satellite Centre jana. Mradi huu una jumla ya nyumba 150 kwa awamu ya kwanza na zitafuata nyumba zingine 150 katika awamu inayofuata.
Meneja wa Miradi ya Ubia, Subira Gudadi akimkaribisha Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Tulia Ackson wakati akiwasili katia eneo la mradi.
Mkurugenzi Mkuu wa NHC, Nehemia Mchechu akijadiliana jambo na Mwenyekiti wa Bodi ya NHC, Mama Blandina Nyoni.
Mkurugenzi Mkuu wa NHC, Nehemia Mchechu, Menyekiti wa Bodi ya NHC, Mama Blandina Nyoni, Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi William Lukuvi na Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Dk. Benilith Mahenge wakimsubiria Mheshimiwa Rais awasili.
Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi William Lukuvi, Mkurugenzi Mkuu wa NHC, Nehemia Mchechu, na Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Dk. Benilith Mahenge wakimkaribisha Mheshimiwa Rais Dk. John Pombe Magufuli.
Rais Magufuli akiwapungia mkono wananchi wakati alipowasili katika eneo la ufunguzi wa nyumba za makazi Iyumbu.
Rais Magufuli akisalimiana na Mshereheshaji wa shughuli hiyo Ephraim Kibonde.



Rais Magufuli akifuatilia baadhi ya mambo.
Baadhi ya wafanyakazi wa NHC wakifuatilia tukio hilo.
Wananchi wakifuatilia tukio hilo la ufunguzi. 
Mkuu wa mkoa Benillith Mahenge akihutubia.
Mkurugenzi Mkuu wa NHC, Nehemia Mchechu, akihutubia.
Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi William Lukuvi akihutubia. 
Rais Magufuli akihutubia katika ufunguzi huo.
Picha ya pamoja.

No comments:

Post a Comment