Foreign Exchange Rates

DStv Advert_090724

DStv Advert_090724

SBT Tanzania Advert_291123

Thursday, 16 November 2017

BCX YATOA ELIMU YA MATUMIZI YA KADI YAKE YA UHURU PAY KWA ABIRIA WA KIVUKONI NA TEGETA-NYUKI

 Mawakala wa Kampuni ya BCX wakiwa katika picha ya pamoja wakijiandaa kutoa elimu ya jinsi ya kutumia mfumo mpya wa kielektroniki wa malipo ya nauli katika usafiri wa Daladala kwa kutumia Kadi au Stika kwa abiria wa eneo la Feri zoezi lililofanyika hivi karibuni jijini Dar es Salaam.
Dereva wa Daladala, Abdallah Kombo akigawa vipeperushi kwa Abiria vinavyoelezea namna ya kutumia mfumo mpya wa malipo ya nauli kielektroniki katika usafiri wa Daladala, uliozindulwa hivi karibuni na Kampuni ya BCX jijini Dar es salaam.

Mawakala wa Kampuni ya Business Connexion (BCX), wakiwahudumia wateja wa huduma mpya ya malipo ya nauli za daladala kielektroniki ijulikanayo kama ‘Uhuru Pay’ katika Kituo cha daladala cha Tegeta Nyuki hivi karibuni jijini Dar es Salaam.
Wakala wa Kampuni ya Business Connexion (BCX), akiwakabidhi vipeperushi wakazi wa Tegeta Nyuki, ambavyo vinatoa maelezo kuhusu huduma mpya ya malipo ya nauli za daladala kielektroniki ijulikanayo kama ‘Uhuru Pay’ iliyozinduliwa na BCX hivi karibuni jijini Dar es salaam.
Mkazi wa Tegeta Nyuki, Bi. Leila Msagar akipewa maelezo kabla ya kusajiliwa na kupewa kadi yake wakati wa uzinduzi wa huduma mpya ya malipo ya nauli za daladala kielektroniki ijulikanayo kama ‘Uhuru Pay’ ambayo ilizinduliwa na BCX hivi karibuni jijini Dar es salaam.

No comments:

Post a Comment