Kampuni ya simu za mkononi ya Tigo, ambayo ni kinara wa ubunifu wa mitindo ya maisha ya kidijitali nchini, imetangaza mageuzi katika uwekezaji ili kuboresha upatikanaji wa mtandao ili kuweza kuwapatia huduma bora zaidi wateja wake wa matumizi ya sauti na data.
Akizungumza na wahariri wa vyombo mbalimbali vya Habari nchini, Ofisa Mtendaji Mkuu wa Ufundi na mawasiliano wa Tigo, Jerome Albou,amesema kampuni hiyo imewekeza kiasi cha dola za kimarekani millioni 75 kwenye mradi mkubwa wa kuendeleza mtandao huo.
Alisema moja ya malengo yao kimkakati ni kubadilisha uzoefu wa wateja kwa kuwapatia mtandao wenye ufanisi kulingana na viwango vya sekta ya mawasiliano ambapo katika miaka mitatu iliyopita Tigo imeweza kuongeza msingi wa wateja wake kufikia zaidi ya milioni 10.
“Kadri tunavyoendelea kukua, kupanua mtandao na kuufanya kuwa wa kisasa zaidi, ni jambo la lazima kutoa huduma bora zaidi,” alisema Albou huku akiongeza kwamba kuanzia mwaka jana kampuni ya Tigo imefanya upanuzi mkubwa wa miundo mbinu ili kuweza kufikia maeneo mengi nchini.
“Mahitaji ya matumizi ya data yamekuwa yakiongezeka kila siku, hivyo Tigo imeweza kuhakikisha matumizi ya 3G na 4G yanaweza kuwafikia watumiaji vijijini,” aliongeza Albou.
No comments:
Post a Comment