Rais Mstaafu wa awamu ya Pili
wa Tanzania Mhe. Ali Hassan Mwinyi (kulia) akipata maelezo kutoka kwa Meneja
wa Data na Vifaa vya intaneti wa Zantel, Hamza Zuheri (wa tatu kushoto) juu ya
huduma mbalimbali zinazotolewa na Kampuni ya Mawasiliano ya Zantel jana jijini
Dar es salaam baada ya kiongozi huyo kutembelea banda la Kampuni hiyo katika
maonyesho ya 41 ya Kimataifa ya Dar es salaam maarufu kama Sabasaba
yanayoendelea hivi sasa katika viwanja vya Mwl J.K Nyerere.
Rais Mstaafu wa awamu ya Pili
wa Tanzania Mhe. Ali Hassan Mwinyi akipata maelezo kutoka kwa Mfanyakazi wa
Zantel Fadhili Mfinanga (wa pili kushoto) juu ya huduma mbalimbali zinazotolewa
na Kampuni ya Mawasiliano ya Zantel jana jijini Dar es salaam baada ya kiongozi
huyo kutembelea banda la Kampuni hiyo katika maonyesho ya 41 ya Kimataifa ya
Dar es salaam maarufu kama Sabasaba yanayoendelea hivi sasa katika viwanja vya
Mwl J.K Nyerere.
Rais Mstaafu wa awamu ya Pili
wa Tanzania Mhe. Ali Hassan Mwinyi (wa pili kulia) akipokea mfuko wa zawadi baada
ya kiongozi huyo kutembelea banda la Kampuni ya Mawasiliano Zantel ili kujionea
huduma mbalimbali zinazotolewa na Kampuni hiyo jana jijini Dar es salaam katika
maonyesho ya 41 ya Kimataifa ya Dar es salaam maarufu kama Sabasaba
yanayoendelea hivi sasa katika viwanja vya Mwl J.K Nyerere. Katikati ni Meneja
wa Data na Vifaa vya intaneti wa Zantel, Hamza Zuheri.
Mkazi wa mkoa wa Morogoro,
Peter Albano akichangia damu katika banda la Kampuni ya Mawasiliano ya Zantel alipotembelea
banda hilo jana jijini Dar es salaam ili kujionea huduma mbalimbali
zinazotolewa na Kampuni hiyo. Zantel kwa kushirikiana na Mpango wa Taifa wa
damu Salama wameandaa utaratibu wa uchangiaji damu kwa ajili ya kuokoa maisha
ya watu wenye uhitaji wa huduma hiyo katika kipindi hiki cha maonyesho ya 41 ya
Kimataifa ya Dar es salaam maarufu kama Sabasaba yanayoendelea katika viwanja
vya Mwl J.K Nyerere. Anayetoa damu ni Msanifu Maabara kutoka Hospitali ya Taifa
ya Muhimbili, Sebastian Magulu.
Mkazi wa Goba, jijini Dar es
salaam, Vincent Xavier akichangia damu katika banda la Kampuni ya Mawasilianao
ya Zantel alipotembelea banda hilo jana jijini Dar es salaam ili kujionea huduma
mbalimbali zinazotolewa na Kampuni hiyo. Zantel kwa kushirikiana na Mpango wa
Taifa wa damu Salama wameandaa utaratibu wa uchangiaji damu kwa ajili ya kuokoa
maisha ya watu wenye uhitaji wa huduma hiyo katika kipindi hiki cha maonyesho
ya 41 ya Kimataifa ya Dar es salaam maarufu kama Sabasaba yanayoendelea katika
viwanja vya Mwl J.K Nyerere. Anayemtoa damu ni Mhudumu wa Afya ya jamii kutoka
Hospitali ya Taifa ya Muhimbili, Erica Ishengoma.
No comments:
Post a Comment