- Wateja wa mtandao wa simu Zantel sasa kufurahia mawasiliano na ndugu jamaa na marafiki waliopo mashariki ya kati kwa bei nafuu kwa kutumia kifurushi cha kimataifa cha uarabuni.
Akitangaza habari hii makao makuu ya kampuni ya Zantel yaliyopo Msasani jijini Dar es salaam Mkurugenzi mkuu wa Zantel Bw. Benoit Janin amesema “Ramadhani ni muda muafaka wa kujenga mahusiano mazuri na ndugu, jamaa na marafiki na ofa hii ni ishara ya Zantel kuwasaidia wateja wake kuweza kuungana na kuwasiliana kwa urahisi zaidi na wapendwa wao”.
Aliongeza kwa kusema mtandao wa Zantel utaendelea kutoa huduma kwa mamilioni ya Watanzania kuwasaidia kutimiza malengo na ndoto zao kupitia vipengele mbali mbali vya huduma za kampuni hiyo ikiwa ni pamoja bidhaa na huduma za upigaji simu, vifurushi vya internet na mtandao. Alisema kampuni itahakikisha vyote hivi kwa kutoa huduma na bidhaa bora za upigaji simu na vifurushi vya intaneti huku tukihakikisha tunawekeza faida endelevu. Kwa mwaka 2016 kulikua na matatizo mbali mbali ila kwa sasa mkakati wetu ni kuhakikisha tunatoa vipao mbele kwa vitu vyenye umuhimu mkubwa kwa wateja ikiwemo kuwa mtandao bora unaotoa intaneti ya kasi zaidi wa 4G, kupenya na kuwafikia watumiaji wengi zaidi,na kujiandaa kwa siku zijazo kuwa kampuni ya bidhaa inayopendwa zaidi.
“Tunahitaji kuwa tayari kwa siku zijazo kwa njia mbali mbali za kuongeza mapato pamoja na huduma zinazoongeza thamani ya mtandao wa zantel ikiwemo uboreshaji wa vifurushi vya intaneti, tayari tunaona mabadiliko makubwa katika mtandao wetu” aliongezea kwa kusema “Kutakua na bidhaa mbali mbali tutakazozitoa kipindi hiki zitakazofurahiwa na wateja wetu kukiwa na mpangilio wa ofa zilizoanza tarehe 24/05/2017” Aliongezea.
Akielezea zaidi kuhusu ofa hii, Mkurugenzi wa masoko wa Zantel Bw. Gasper Mbowa amesema”Ofa hii ya Ramadhani imelenga kuwazawadia wateja wetu wa malipo ya kabla watakaojiunga na vifurushi vyetu kwa kiasi chochote au kwa kuongeza muda wa maongezi kwenye kipindi cha mfungo wa Ramadhani. Mteja yoyote atakayeongeza mda wa maongezi atapata asilimia 50 ya muda wa maongezi moja kwa moja utakaomuwezesha kupiga simu Zantel kwenda Zantel, ofa hii itakua inatumika kuanzia saa 5 usiku hadi saa 12 asubuhi. Vivyo hivyo wateja wataweza kutumia huduma zetu zilizozinduliwa hivi karibuni kama ‘Zantel madrassa itakayowawezesha kujifunza dini ya kiislamu kwa kupokea mafunzo ya Quran, hadith, dua, habari za BAKWATA na huduma nyingine nyingi kwa kupitia simu zao za mkononi kupitia ujumbe mfupi wa maneno au kwa kupiga simu.
Mbowa aliongezea kuwa wateja wa Zantel wanaweza kuwapigia simu ndugu, jamaa na marafiki waliopo mashariki ya kati kwa bei nafuu zaidi kupitia kifurushi cha kimataifa cha uarabuni. “Kwa shilingi za kitanzania 2,000 wateja watapata dakika 4 za kupiga simu Qatar, Oman, UAE, Lebanon, Pakistan, Yemen & Saudi Arabia, na kwa shilingi 5,000 watapata dakika 7 kupiga simu kwenda kwenye nchi tajwa, na fedha hizo zitakatwa moja kwa moja kwenye akaunti zao”
Vifurushi vyote hivi vitapatikana kwa kujiunga kwa kupiga *149*15# na kwa vifurushi vya ‘Bonga Mpakabasi’, ‘Zantel Madrassa’ wateja wataweza kujiunga kwa kutuma ujumbe wa maneno kwa kutumia neno SUB na kutuma kwenda namba 15586 au kwa kupiga namba 15586
Mtaalamu wa habari: Rukia Mtingwa
Barua pepe: r.mtingwa@zantel.co.tz
Tovuti: www.zantel.com
Kuhusu Zantel
Mtandao wa Mawasiliano wa Zanzibar (Zantel) ni miongoni mwa wawekezaji na wagunduzi kwenye sekta ya mawasilino wakiongoza kwa utoaji wa huduma bora kwa wateja. Lakini zaidi ya yote, ni miongoni mwa kampuni ya mawasiliano inayokuwa kwa kasi kubwa na inayotengeneza faida kubwa katika Sekta ya mawasiliano Tanzania. Mtandao huu wa Mawasiliano Zanzibar ndiyo mtandao pekee wa huduma za mawasiliano unaotoa huduma ya simu za nje kwa bei nafuu, simu na bando kupitia mfumo bora wa CDMA, GSM, 3G networks.
Huduma za Zantel zimekuwa zikikua kutokana na kuongezeka watumiaji wake huku ikizidi kuonyesha ubora katika huduma zake ambazo kila mtu anaweza kuzimudu pamoja na kutoa huduma ya haraka ya mtandao wa wireles kwa haraka na ubora.
Zantel imepokea tuzo mbalimbali kutokana na kutambuliwa kutoa huduma bora na ufumbuzi kwenye sekta ya mawasilino. Baadhi yake ni pamoja na Tuzo ya GSMA M – Health. Zantel imedhamiria kuwaunganisha watu ulimwenguni ili wawe mstari wa mbele kupata tarifa kwa haraka.
Kwa maelezo zaidi tafadhali, tembelea tovuti yetu…www.zantel.com
No comments:
Post a Comment