Kwa mujibu wa Tigo kampeni ya ‘Jaza Ujazwe’ imekuja kama shukrani kwa wateja wa kampuni hiyo ya simu kutokana na uaminifu wao mkubwa.
Akizungumza wakati wa uzinduzi wa kampeni hiyo, Meneja Chapa wa Tigo, William Mpinga alisema, “Tigo inathamini kuungwa mkono kulikotukuka kunakoonyeshwa na wateja wake kwa kipindi cha miaka mingi, na ndio maana tunaamini wanastahili kupewa shukrani kwa kuendelea kutuamini. Kama kampuni, tunayofuraha kwa mara nyingine tena kuwapatia wateja wetu bonus ili waweze kuendelea kufurahia huduma zetu za kiwango cha juu duniani.”
Mpinga alibainisha kuwa kampeni hiyo mpya inadhihirisha nafasi ya kampuni katika kutoa huduma na bidhaa bora zinazokidhi mahitaji ya wateja wake na wakati huo huo kuimarisha mchango wake katika soko kama kampuni ya simu za mkononi iliyo na ubunifu wa hali ya juu.
Alisisitiza kujikita kwa Tigo katika kuendelea kuwapatia wateja wake bidhaa na huduma bora zaidi na kuongeza, “Bidhaa na huduma zetu zimeundwa baada ya kufanya tafiti zinazolenga kuhakikisha wateja wetu wanaridhishwa na wanapata thamani kwa kila shilingi wanayotumia kwa mawasiliano. Hivyo ‘Jaza Ujazwe’ ni kuitikia hitaji la mteja na pia kuwapa wateja uzoefu wa kusisimua kila wakati wanapotumia bidhaa zetu. Tunaamini kwamba wateja wetu watafurahia dakika za ziada, ujumbe mfupi wa maneno (SMS) au data za bonus na hatimaye kuboresha mwenendo wao wa mawasialiano.
Wateja wote wa Tigo wanastahili kupata bonus hizi kwa kuwa hakuna masharti yoyote.
No comments:
Post a Comment