Kutoka kushoto, Wakurugenzi Raymond Mdolwa, Haikamen Mlekio, Fatuma Chillo, Hamad Abdallah na Felix Maagi wakifuatilia hotuba ya Waziri Lukuvi wakati wa uzinduzi wa Bodi Mpya. |
Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi William Vangimembe akizungumza na wajumbe wapya wa Bodi ya Wakurugenzi wa NHC wakati wa uzinduzi wa Bodi mpya ya Shirika la Nyumba la Taifa (NHC). |
Wajumbe wapya wa Bodi ya Wakurugenzi ya NHC na Menejimenti ya NHC pamoja na Waziri wakiwa katika picha ya pamoja. |
Wajumbe wapya wa Bodi ya Wakurugenzi ya NHC na Menejimenti ya NHC pamoja na Waziri wakiwa katika picha ya pamoja. |
Waziri Lukuvi ameyasema hayo kwenye Makao Makuu ya Shirika la Nyumba la Taifa, NHC PLACE hivi karibuni kwa kuitaka Bodi hiyo ilisimaie Shirika hilo kwa maslahi ya Taifa huku ikihakikisha kuwa halipati hasara.
"Nataka NHC ijenge nyumba kwaajili ya watu masikini kwa bei na ubora, mbuni mikakati yenye kuzingatia hili ili watanzania wengi zaidi waweze kumiliki nyumba bora. Simamieni misingi. Bodi mpate muda wa kuwasikiliza wapangaji. Ujenzi wa nyumba za gharama nafuu uongeze kasi mfafanue suala hili katika sera yenu kila mtu ajue nyumba ya gharama nafuu maana yake nini," alisema.
Alilitaka Shirika la Nyumba la Taifa ujenzi wa gharama nafuu uzingatiwe kama ilivyoelezwa kwenye Ilani ya Uchaguzi ya Chama tawala kwa kuzifanya ziwe na bei nafuu kwa Watanzania wa kipato cha chini ziwe bora na kuwaletea wananchi maisha bora kwa kupitia nyumba.
"Rais ameshatoa maelekezo kuwa popote NHC inapojenga nyumba pawekewe miundombinu husika na Halmashauri na mamlaka zingine husika kama Tanesco na Maji na ardhi iwepo ya bure na ndiyo maana pale kwenye mradi wa Iyumbu Dodoma, Rais ameahidi kuagiza huduma zitolewe bure.
Alisema anafahamu kuwa NHC inajenga nyumba za biashara iendelee na kazi hiyo bila kuzikwaza zile za gharama nafuu.
"Najua NHC mnajenga nyumba za biashara fanyeni tu ili mradi hampati hasara. Mjikite katika kubuni teknolojia za kisasa zitakazoweza kupunguza gharama. Mjifunze aina mbalimbali za teknoljia. Jengeni mahusiano na idara mbalimbali za serikali. Tumewapa status kama Master Developers ili muwe champion wa upangaji wa miji fanyeni hivyo tofauti ionekane," alisema.
Alilitaka Shirika lianzishe kitengo cha kupanga na kupima Ardhi ili kupunguza ujenzi holela na kuiagiza NHC kujenga Miradi midogo midogo yenyewe kwani Kama Shirika ni Mkandarasi wa Daraja la Kwanza "Jengeni wenyewe ili muwe mfano bora kwa makandarasi. Ningependa Bodi mlifanye Shirika liwe stable kwa kuweka ubunifu wenu."
Aliongeza kwa kuitaka Bodi hiyo mpya ijihusishe na usikilizaji wa malalamiko na migogoro yote ya wapangaji kwa kuzingatia sheria zilizopo.
“Mshiriki kikamilifu kujenga nyumba Makao Makuu Dodoma ili kuisaidia Serikali kuhamia Dodoma kupunguza upungufu wa makazi ziwe za kuuza na au kupangisha. Kamilisheni miradi mliyoanza msijipanue sana kabla ya kumaliza miradi mikubwa.
Bodi hiyo inaongozwa na Mwenyekiti wake Mama Blandina Salome Joseph Nyoni na wajumbe Prof. John M. Lupala, Gabriel Malata, Mary Mlay, Subira Mchumo, Ally Hussein Laay, Pius Maneno na Injinia Kesogukwele Masudi Issa Miraji Msita.
No comments:
Post a Comment