Mkuu wa kitengo cha Masoko na Ubunifu wa Kampuni hiyo, Deogratius Lazari Mosha.
Kampuni ya Maxcom Africa (Maxmalipo)
inawakaribisha watanzania kushiriki manunuzi ya hisa za makampuni
yaliyoorodheshwa kwenye Soko la hisa la Dar es salaam(DSE) kwa njia ya mtandao
(simu za kiganjani) na kufanya malipo kupitia kwa mawakala wa Maxmalipo waliopo
nchi nzima Tanzania.
Mkuu wa kitengo cha Masoko na Ubunifu wa Kampuni
hiyo, Deogratius Lazari Mosha, amewaambia waandishi wa habari jijini Dar es
salaam leo kwamba Maxcom Africa (Maxmalipo) ikishirikiana na soko la hisa la
Dar es Salaam (DSE) kwa kutumia mfumo madhubuti wa simu za viganjani
unamwezesha Mtanzania kuweza kushiriki kwenye Manunuzi ya hisa za makampuni
yaliyoorodheshwa kwenye soko la awali la mitaji (primary markets ) kwa kupiga
*150*36#, ameongeza kwamba baadhi ya makampuni hayo kwa sasa ni Vodacom na
TCCIA.
Akifafanua hili, Lazari amesema ili Mtanzania aweze kushiriki Manunuzi ya hisa kwa mfumo huu anatakiwa kubonyeza *150*36# kisha ataingia kwenye Menyu ya soko la hisa na Kuchagua IPO kisha atachagua kampuni anayotaka kununua hisa, baada ya kufanya hivyo mteja atalazimika kujisajili na kisha atapata nafasi ya kuainisha idadi ya hisa anazohitaji(zisizo pungua 100 katika awamu ya kwanza).
Lazari ameongeza kwamba baada ya hatua ya
uanishaji wa hisa, mteja atapokea ujumbe mfupi wa simu kutoka DSE wenye nambari
ya kumbukumbu ya malipo, idadi ya hisa na kiasi anachotakiwa kulipia. Ili
kukamilisha malipo haya mteja atatakiwa kufika kwa wakala yeyote wa Maxmalipo
aliye karibu naye na kufanya malipo kama ilivyo ainishwa kwenye ujumbe
aliopokea kwenye simu yake. Mteja anahimizwa kuhakikisha kwamba anapatiwa
risiti pindi anapolipia hisa kwa mawakala wa Maxmalipo ili kutunza kumbu kumbu
zake.Akifafanua hili, Lazari amesema ili Mtanzania aweze kushiriki Manunuzi ya hisa kwa mfumo huu anatakiwa kubonyeza *150*36# kisha ataingia kwenye Menyu ya soko la hisa na Kuchagua IPO kisha atachagua kampuni anayotaka kununua hisa, baada ya kufanya hivyo mteja atalazimika kujisajili na kisha atapata nafasi ya kuainisha idadi ya hisa anazohitaji(zisizo pungua 100 katika awamu ya kwanza).
Kwa kuongezea, Lazari ameeleza kwamba mfumo huu
rafiki unamwezesha mteja kushiriki manunuzi ya hisa kadiri ya uwezo wake
(Mfano, Mteja Anaweza kila siku akanunua hisa 100 kulingana na kipato chake au
zaidi). Pamoja na mwakala wa Maxmalipo mteja anaweza kulipia kwa kutumia
mitandao ya simu.
Mfumo huu wa kununua hisa kwa simu za kiganjani (
*150*36#) umetengenezwa na kampuni ya kitanzania ya Maxcom Africa (Maxmalipo)
ikishirikiana na Soko la hisa la Dar es Salaam(DSE) na ni mfumo rasmi wa kuuza
na kununua hisa kwenye soko la hisa.
Watanzania wamepewa wito wa kushiriki ununuzi wa hisa kwa njia ya simu ya kiganjani na kuhakikisha wanafanya malipo mapema kupitia kwa mawakala wa Maxmalipo walioko nchi nzima takribani Mawakala Elfu kumi na sita .
Watanzania wamepewa wito wa kushiriki ununuzi wa hisa kwa njia ya simu ya kiganjani na kuhakikisha wanafanya malipo mapema kupitia kwa mawakala wa Maxmalipo walioko nchi nzima takribani Mawakala Elfu kumi na sita .
No comments:
Post a Comment