Foreign Exchange Rates

DStv Advert_090724

DStv Advert_090724

SBT Tanzania Advert_291123

Thursday, 10 November 2016

TTCL YAWAFUATA WATEJA MTAANI

KAMPUNI ya Simu Tanzania TTCL, leo imeanza Kampeni ya kuwafuata wateja wake mitaani ili kuzungumza nao, kuwapa taarifa za huduma zinazotolewa na kuwaunganisha wateja hao katika huduma mbali mbali za TTCL. 

Kampeni hiyo imeongozwa na Kaimu Afisa Mtendaji Mkuu wa TTCL Bw Waziri W. Kindamba na kusaidiwa na Wakuu wa Idara na Vitengo pamoja na Wafanyakazi wa TTCL waliosambaa katika maeneo mbali mbali ya Jiji la Dar Es Salaam. "Huu utakuwa ni utamaduni wetu, tutawafuata Wateja popote walipo, tutawapa taarifa za huduma zetu bora na nafuu, tutawasikiliza na kufanyia kazi maoni yao.

Tunataka kuwahakikishia Wananchi kuwa, hii ni TTCL Mpya, Shirika lao la kizalendo limerejea katika nafasi ya mhimili mkuu wa Mawasiliano nchini Tanzania. Watumie huduma zetu, waone tofauti, wapate ubora na viwango vya juu kabisa", amesema Bw Kindamba. 

Kwa upande wake Afisa Mkuu wa Masoko na Mauzo wa TTCL Bw Peter Ngota amesema, TTCL inawaletea wateja wake Ofa MPYA kabambe kwa ajili ya Simu ya Mezani inayotoa uhakika wa mawasiliano kati ya Wanafamilia.

Kwa Mteja atakayeongeza salio la shilingi 23,000/- atapata ofa ya Simu Bure pamoja na ofa kupiga simu TTCL kwenda TTCL bure.

No comments:

Post a Comment