Pamoja na kuwepo kwa maendeleo ya kasi katika nyanja mbalimbali lakini sekta ya teknolojia inabaki kuwa moja ya njia ambayo imechangia kwa kiasi kikubwa kupatikana kwa mafanikio hayo kwa kurahisisha kazi nyingi kufanyika kwa haraka.
Kwa kutambua hilo, kampuni inayohusika na utoaji wa huduma zinazohusiana na teknolojia ya EnGenius imeingia katika makubaliano na kampuni ya usambazaji wa vifaa vya kiteknolojia ya Red Dot ili iweze kusambaziwa vifaa na huduma mbalimbali ambazo zinafanywa na Red Dot katika nchi za Afrika Mashariki.
Kampuni ya EnGenius ambayo inatoa huduma kama za internet wireless, radio frequency (RF) technology na kusambaza bidhaa mbalimbali kama kompyuta imesema kuwa imefanya maamuzi ya kuingi katika makubaliano na Red Dot ikiamini kuwa ni moja ya njia sahihi ambayo itawawezesha kuwafikia wateja kwa karibu zaidi.
Akizungumzia makubaliano hayo, Mkuu wa Kanda wa EnGenius, Van Hsiao alisema kampuni ao kwa sasa inahitaji kujitanua katika nchi za Afrika Mashariki kama Tanzania, Kenya, Uganda, Rwanda na Ethiopia hivyo wameungana na Red Dot ili waweze kukuza biashara yao zaidi.
"Tumeingia makubaliano na moja ya wasambazaji wakubwa wa Red Dot na tunaamini watatusaidia EnGenius kufikia malengo yetu ya kuwa wauzaji wakubwa wa bidhaa za kiteknolojia kwa Afrika Mashariki, tunafahamu kuwa ni wasambazaji wakubwa na atatusaidia kukuza biashara yetu," alisema Hsiao.
No comments:
Post a Comment