Mara baada ya ndege inayozinduliwa kuwasili katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Julius Nyerere, ililakiwa na mizinga ya maji kama ishara ya heshima kubwa na abiria walioshuka wakikaribishwa kwa burudani ya ngoma za kitamaduni za Tanzania.
Shughuli ya kukata utepe ilifuatia ambayo katika kuweka kumbukumbu ya tukio hilo la kufana ambapo lilifanikishwa na
- Dr Shaaban Mwinjaka, Katibu Mkuu, Wizara ya Uchukuzi
- Dr Adelhelm James Meru, Katibu Mkuu Wizara ya Utalii na Maliasili
- H.E. Mbarouk Nassor Mbarouk, Balozi wa Tanzania Nchi za Falme za kiarabu
- H.E. Abdullah Ibrahim Al Suwaidi, Balozi wa Nchi za Falme za kiarabu Tanzania
- Daniel Barranger, Makamu wa Rais wa Mauzo ya kimataifa wa shirika la ndege la Etihad
- Mhandisi:Thomas Haule Mkurugenzi Mamlaka ya Ndege
Dar es Salaam imekuwa ni kituo cha tatu kwa shirika la ndege la Etihad Afrika Mashariki, baada ya Nairobi na Entebbe, na ya tisa barani Afrika.
Huduma hii mpya ikiwa inaendeshwa na ndege aina ya Airbus A320 yenye madaraja mawili, siti 16 daraja la “Business” na siti 120 daraja la “Economy” ikiwa imelenga wafanya biashara na wanaosafiri kwa starehe moja kwa moja kila siku baina ya Dar es salaam na Abu Dhabi, pamoja na uunganishaji mrahisi kwenda nchi nyingine ukanda wa GCC, Ulaya, India, Asia kaskazini, Asia ya Kusini na Australia.
Bw. Barranger, alisema “uzinduzi huu wa safari za shirika la ndege la Etihad kuja Dar es Salaam zimewiana na mkakati wetu wa kulenga masoko yanayo endelea kukua kwa kasi”.
“Dar es Salaam ni mji ambao umekuwa kivutio sana kwa watalii wanaotaka kufahamu tamaduni na historia ya Tanzania, pia ni mlango wa vivutio vya kitalii vingi vya kitaifa na kimataifa ikiwemo mlima Kilimanjaro, mbuga za wanyama kama Serengeti na kisiwa cha Zanzibar.
“Nchi Falme za kiarabu ni mdau mkubwa wa kibiashara na Tanzania, huduma hii mpya itaongeza nguvu ushirikiano wa kibiashara baina ya nchi hizi mbili. Ratiba za safari za ndege zitawapa wageni urahisi wa kupata ndege za kuunganisha safari kwenda nchi nyingine, ikiwa inahudumia safari nyingi sana baina ya Tanzania na nchi nyingi katika mtandao wetu wa kimataifa kama Ahmedabad na Mumbai nchini India au Beijing na Shanghai nchini China.”
“Pamoja na kutoa huduma ya moja kwa moja kwa watalii na wafanya biashara baina ya nchi hizi mbili, safari hizi pia zimeendelea kuimarisha uwepo wetu Afrika Mashariki na Afrika kwa ujumla” aliongezea.
Shirika la ndege la Etihad limekuwa likiongeza uwepo wake barani Afrika tokea walipozindua safari zake za kwanza barani Afrika, huko Cairo November 2004. Baada ya hapo zikafuatia Casablanca, Entebbe, Johannesburg, Khartoum, Lagos, Nairobi, (15 January 2015) na Mahe huko visiwa vya shelisheli na mipango ya uzinduzi katika mji wa Rabat, Morocco katikati ya mwezi Januari 2016.
Flight No.
|
Kutoka
|
Kuondoka
|
Kwenda
|
Kufika
|
Idadi
|
Ndege
|
EY681
|
Abu Dhabi (AUH)
|
8:20
|
Dar es Salaam (DAR)
|
13:00
|
Kila Siku
|
A320
|
EY682
|
Dar es Salaam (DAR)
|
13:50
|
Abu Dhabi (AUH)
|
20:15
|
Kila Siku
|
A320
|
Ratiba za shirika la ndege la Etihad, Dar es Salaam kuanzia tarehe 1 December 2015:
Kuhusu Shirika la Ndege la Etihad
Shirika la Ndege la Etihad lilianza shughuli zake mnamo mwaka 2003na hadi kufikia mwaka 2014, ilikuwa limeshabeba abiria takriban milioni 14.8. Kutoka makao makuu yake huko Abu Dhabi, shirika hili linasafiri au limetangaza mipango ya kuhudumia wasafiri na mizigo kutoka vituo 116 huko Mahariki ya kati, Afrika, Ulaya, Asia, Australia na nchi za Americas. Shirika lina ndege aina ya Airbus na Boeing takriban 120, Zaidi ya ndege 200 zikiwa zimewekea oda, zikiwemo Boeing 787s 66, Boeing 777Xs 25, Airbus A350s 62 na Airbus A380s tano.
Shirika la Etihad pia limewekeza katkia AirBerlin, Air Serbia, Air Seychelles, Alitalia, Jet Airways , Virgin Australia, pamoja na shirika lenye makazi Uswiss Darwin Airline, likifanya biashara kama Etihad Regional. Shirika la Ethihad, sambamba na airberlin, Air Serbia, Air Seychelles, Alitalia, Etihad Regional, Jet Airways na NIKI, pia hushiriki pamoja nkwatika washirika wa Etihad Airways, brand mpya inayowaleta kwa pamoja mashirika mengine ya ndege yenye uelewa sawa ili kutoa huduma bora zaidi kwa wateja, kuwapa wateja ratiba nzuri Zaidi na kuwazawadia wateja wakudumu.kwa maelezo Zaidi, tafadhali tembelea :www.etihad.com
Kwa maelezo zaidi wasiliana na:
Damian James, Meneja Mahusiano Shirika la Ndege la Etihad
Simu: + 971 2 511 1035 / Barua pepe: djames@etihad.ae
No comments:
Post a Comment