| Meneja Usalama na Mazingira wa Kampuni ya Saruji Tanga (Simba Cement), Leon Breedt (wa pili kulia), akikabidhi sehemu ya msaada wa mifuko 160 ya saruji kwa Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi Mikanjuni ya mjini Tanga, Grayso Mnyumba, kusaidia uboreshaji wa mazingira ya shule, katika hafla iliyofanyika eneo la kiwanda, Pongwe, Tanga mwishoni mwa wiki. Wengine ni wafanyakazi wa saruji na kutoka shule ya Mikanjuni. Kampuni hiyo kupitia mpango wake wa kusaidia jamii (CSR) kwa mwaka huu imeshatumia kiasi cha shs 46,651,120 kusaidia katika maeneo ya elimu, afya, maendeleo ya jamii na mazingira sehemu mbalimbali nchini. |
No comments:
Post a Comment