Foreign Exchange Rates

DStv Advert_090724

DStv Advert_090724

SBT Tanzania Advert_291123

Sunday, 12 July 2015

BENKI YA NBC YAFUTURISHA WATEJA WAKE MJINI ZANZIBAR

Mkuu wa Kitengo cha Huduma za Kibenki zinazofuata misingi na kanuni za Kiislamu cha Benki ya NBC, Yassir Masoud (kushoto), Mkuu wa Kitengo cha Wateja Binafsi cha benki hiyo, Musa Jallow na Ofisa Fedha Mkuu wa NBC, Jaffari Matundu (kushoto) wakishiriki kuchukua mlo wa futraru pamoja na baadhi ya wateja wa benki hiyo mjini Zanzibar katika hafla ya futari iliyoandaliwa na NBC kwa wateja wake mjini humo juzi.
Mkuu wa Kitengo cha Wateja Binafsi wa Benki ya NBC, Musa Jallow (kushoto), akishikana mikono na Mkurugenzi Idara ya Elimu Maandalizi na Msingi wa Zanzibar, Bi Safia Ali Rijal wakati wa hafla ya futari iliyoandaliwa na NBC kwa ajili ya wateja wao wa Zanzibar. Halfa hiyo ilifanyika visiwani humo. Wa pili kushoto ni Waziri wa Kilimo na Maliasili wa Zanzibar, Dk. Sira Mamboya na Ofisa Fedha Mkuu wa benki hiyo, Jaffari Matundu.
Mwenyekiti wa Bodi ya Benki ya NBC, Dk. Kassim Hussein akihutubia katika hafla ya futari iliyoandaliwa na benki hiyo kwa ajili ya wateja wake wa Zanzibar iliyofanyika visiwani humo.
Waziri wa Kilimo na Maliasili wa Zanzibar, Dk. Sira Mamboya akizungumza katika hafla hiyo ambapo aliipongeza benki ya NBC kwa kuboresha huduma za kibenki kwa kupitia dirisha la Islamic Banking visiwani humo.
Baadhi ya wateja wa Benki ya NBC visiwani Zanzibar wakishiriki futari iliyoandaliwa na benki yao mjini humo juzi.
Ofisa Fedha Mkuu wa NBC, Jaffari Matundu akizungumza katika hafla hiyo.
Baadhi ya wateja wa NBC na wageni wengine waalikwa wakichukua mlo wa futari iliyoandaliwa na benki hiyo.
Baadhi ya wateja wa Benki ya NBC visiwani Zanzibar na wageni wengine waalikwa wakishiriki futari iliyoandaliwa na benki hiyo mjini humo juzi.

No comments:

Post a Comment