Na Mwandishi wetu, Dodoma
KONGAMANO kubwa la siku mbili la kujadili namna taifa linavyojiandaa kutekeleza malengo mapya ya Maendeleo endelevu (SDGs) limefanyika mwishoni mwa wiki mjini Dodoma.
Kongamano hilo lililoandaliwa na Taasisi ya Utafiti ya Masuala ya Uchumi na jamii (ESRF) limelenga kuwakutanisha wataalamu kutoka Tanzania Bara na Visiwani kujadili namna ya kupata fedha za kutekeleza malengo hayo baada ya kumalizika kwa malengo ya maendeleo ya millennia (MDG’s) baadae mwaka huu.
Miongoni mwa mambo yaliyojadiliwa katika kongamano hilo ambapo wataalamu wa Umoja wa Mataifa wa maendeleo walishiriki ni pamoja na namna ya kupata fedha kwa ajili ya maendeleo baada ya Septemba mwaka 2015 kwa kuangalia rasilimali za ndani.
Mada hiyo imetokana na ukweli kuwa upatikanaji wa fedha za ndani ndio suluhu ya utekelezaji wa malengo mapya kwa kuwa awali kwenye MDG’s utekelezaji wa malengo ulikwamishwa na kukosekana kwa fedha kutoka kwa wafadhili ambao waliahidi kuchangia maendeleo.
Pamoja na kuangalia upatikanaji wa fedha kutekeleza malengo hayo mapya bila kuacha yale ya zamani, washiriki pia waliangalia namna ya kujiandaa katika ufuatiliaji wa malengo ya Maendeleo endelevu (SDG’s).
Mkurugenzi Mtendaji mpya wa Taasisi Huru ya Utafiti wa Uchumi na Jamii (ESRF), Dk. Tausi Kida, akitoa maelezo ya kongamano kabla ya kumkaribisha mgeni rasmi kulifungua katika ukumbi wa mikutano hoteli ya St Gasper mjini Dodoma alisema kuwapo kwa kongamano hilo kumetokana na haja ya kujiandaa kabla ya mkutano wa tatu wa namna ya kutafuta fedha kwa ajili ya miradi ya maendeleo.
Mkutano huo utafanyika mwezi ujao mjini Addis Ababa, Ethiopia.
Aidha alisema kwamba upo umuhimu wa kuangalia uimarishaji wa ushirikiano wa dunia katika kuimarisha maendeleo endelevu.
Dk. Kida alisema kwamba kongamano hilo ambalo ni sehemu ya maandalizi ya kuingia katika SDGs; na kuwa taasisi ya ESRF kwa miaka mitatu imekuwa likifuatilia katika kuratibu mazungumzo kuhusu hatima yam MDG’s baada ya 2015.
Akifungua mkutano huo Katibu mkuu Hazina Dk. Servacius Likwelile aliwataka washiriki kuhakikisha kwamba wanachambua masuala muhimu yanayohusu maendeleo na kuyawekea mkakati katika mkutano ujao wa Addis Ababa, Ethiopia.
Akisoma hotuba kwa niaba ya Katibu Mkuu, Kamishina wa Fedha kutoka Nje Wizara ya Fedha Ngosha Magonya amesema kwamba amefurahishwa na juhudi za ESRF kuwakutanisha wataalamu kujipanga kwa mikutano ijayo na utekelezaji wa maendeleo endelevu ya SDG’s.
Aidha aliipongeza taasisi ya United Nations Development Programme (UNDP) kwa kusaidia Tanzania kuangalia hali ilivyokuwa katika MDG’s na hali ya baadae.
Kamishna wa Fedha za Nje wa Wizara ya Fedha, Ngosha Magonya akisoma hotuba ya ufunguzi wa kongamano hilo kwa niaba ya mgeni rasmi Katibu Mkuu wa wizara hiyo katika hoteli ya St. Gasper mwishoni mwa wiki mjini Dodoma.
Mtaalamu wa masuala ya uchumi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) Dar es salaam, Rogers Dhliwayo akitoa salamu za Shirika la Umoja wa Mataifa la Maendeleo (UNDP) wakati wa kongamano hilo la siku mbili la kujadili namna taifa linavyojiandaa kutekeleza malengo mapya ya Maendeleo endelevu (SDGs) lililofanyika mwishoni mwa wiki mjini Dodoma.
Afisa Mwandamizi wa uhamasishaji na uwekezaji kutoka kituo cha uwekezaji nchini (TIC), Lilian Mwamdanga akishiriki kuchangia maoni wakati kongamano kubwa la siku mbili la kujadili namna taifa linavyojiandaa kutekeleza malengo mapya ya Maendeleo endelevu (SDGs) limefanyika mwishoni mwa wiki mjini Dodoma.
Naibu Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP)- Programme, Amon Manyama akichangia maoni wakati wa kongamano kubwa la siku mbili la kujadili namna taifa linavyojiandaa kutekeleza malengo mapya ya Maendeleo endelevu (SDGs) limefanyika mwishoni mwa wiki mjini Dodoma.
Mkurugenzi Mtendaji mpya wa Taasisi Huru ya Utafiti wa Uchumi na Jamii (ESRF), Dk. Tausi Kida na Kamishna Mipango wa Tume ya Mipango Zanzibar, Ahmed Makame Haji wakifuatilia kwa umakini maoni mbalimbali ya wadau yaliyokuwa yakitolewa kwenye kongamano hilo.
Pichani juu na chini ni washiriki kutoka Tanzania bara na visiwani walioshiriki kongamano hilo la siku mbili ambalo liliandaliwa na taasisi ya ESRF.
Mkurugenzi Mtendaji mpya wa Taasisi Huru ya Utafiti wa Uchumi na Jamii (ESRF), Dk. Tausi Kida (kushoto) akimsindikiza Kamishna wa Fedha za Nje wa Wizara ya Fedha, Ngosha Magonya ambaye alimwakilisha mgeni rasmi Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha mara baada ya kufungua kongamano kubwa la siku mbili la kujadili namna taifa linavyojiandaa kutekeleza malengo mapya ya Maendeleo endelevu (SDGs) limefanyika mwishoni mwa wiki mjini Dodoma.
No comments:
Post a Comment