Foreign Exchange Rates

DStv Advert_090724

DStv Advert_090724

SBT Tanzania Advert_291123

Wednesday, 17 June 2015

KAMPUNI ZAIDI TANZANIA ZAJIUNGA KATIKA VITA DHIDI YA KUITOKOMEZA MALARIA

Wadau kutoka kampuni mbali mbali akiwemo Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Dr. Seif Rashid Suleiman na aliyekua Rais wa Chama cha Mpira (TFF), na Balozi wa Malaria Safe, Leodegar Tenga, katika mkutano wakujadili jinsi ya kuitokomeza malaria uliofanyika katika hoteli ya Coral Beach, jijini Dar es Salaam hivi karibuni.
Mkurugenzi Mkazi wa USAID Tanzania, Bi. Sharon Cromer, akiongea na wadau wa kampuni mbalimbali (hawapo pichani), kuhusu umuhimu wakujiunga na kampuni zingine kupambana dhidi ya kuitokomeza malaria nchini Tanzania katika mkutano uliofanyika katika hoteli ya Coral Beach, jijini Dar es Salaam hivi karibuni.
Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Dr. Seif Suleiman Rashid, akiwahutubia wadau wa kampuni mbalimbali (hawapo pichani), alipozikaribisha kampuni 28 zilizokubaliani kujiunga na kampuni zingine kupambana dhidi ya kuitokomeza malaria nchini Tanzania.
Wadau wa kampuni mbali mbali kutoka kampuni zilizo jiunga katika vita dhidi ya kuitokomeza malaria, katika picha ya pamoja.
Bwana Nicholus Nderungo (kushoto) kutoka John Hopkins, Center for Communication Programs na Dr. John kutoka kampuni ya BG Tanzania wakiwa katika picha ya pamoja.

No comments:

Post a Comment