Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mhe. Bernard K. Membe (Mb.) akifungua rasmi Mkutano wa Baraza la Mawaziri wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) uliofanyika kwenye Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNICC) Jijini Dar es Salaam tarehe 30 Mei, 2015. Mkutano huo ambao ni maandalizi ya Mkutano wa Wakuu wa Nchi wa EAC utakaofanyika tarehe 31 Mei, 2015, pamoja na mambo mengine utapokea na kujadili taarifa zitakazowasilishwa na Jopo la Watu Maalum wanaofuatilia hali ya siasa na usalama nchini Burundi, Taarifa ya Wanasheria Wakuu kutoka Nchi Wanachama na Taarifa ya Mawaziri waliotembelea nchini Burundi hivi karibuni kwa ajili ya kutathmini hali. Kulia ni Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Afrika Mashariki, Dkt. Richard Sezibera. |
No comments:
Post a Comment