Foreign Exchange Rates

DStv Advert_090724

DStv Advert_090724

SBT Tanzania Advert_291123

Saturday, 23 May 2015

MKUTANO NA MKURUGENZI MKUU WA IDARA YA HABARI NA DIPLOMASIA KWA UMMA KUTOKA WIZARA YA MAMBO YA NJE YA INDONESIA

Mkurugenzi Idara ya Asia na Australasia Balozi Mbelwa Kairuki akimkaribisha Mkurugenzi Mkuu wa Idara ya Habari na Diplomasia kwa Umma kutoka Wizara ya Mambo ya Nje ya Ndonesia Balozi Esti Andayane. Balozi Kairuki pamoja na mgeni wake walikutana kwa mazungumzo yaliyo jikita katika kukuza Ushirikiano kati ya Tanzania na Indonesia kwenye nyanja mbalimbali za Kiuchumi.
Balozi Kairuki akimsikiliza Balozi Esti Andayane wakati wa mazungumzo.
Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali Bi. Mindi Kasiga (wa kwanza kushoto), katikati Afisa Mambo ya Nje Khatibu Makenga na wakwanza kulia ni Dora Lucas Maina akiwa katika Elimu ya Vitendo.
Ujumbe ulioambatana na Balozi Esti Andayane nao wakisikiliza mazungumzo kati ya Balozi Kairuki na Balozi Andayane (hawapo pichani).
Mazungumzo yakiendelea.
Picha ya pamoja baada ya mazungumzo.
Balozi Mbelwa Kairuki, Mkurugenzi wa Idara ya Asia na Australia amekutana na kufanya mazungumzo na Mkurugenzi Mkuu wa Habari na Diplomasia ya Umma (Director General for Information and Public Diplomacy) kutoka Wizara ya mambo ya Nje ya Jamhuri ya Indonesia, Balozi Esti Andayane.

Katika mazungumzo yao, Mabalozi hao wamekubaliana kukuza ushirikiano baina ya Indonesia na Tanzania katika nyanja za uchumi. Balozi Andayane ameelezea utayari wa Indonesia kuendelea kuisaidia Tanzania katika sekta ya Kilimo kwa kutoa fursa za mafunzo kwa ajili ya wataalam wa kilimo nchini. 

 Tayari Indonesia imeisaidia Tanzania kwa kujenga Kituo cha Utafiti wa Kilimo kilichopo Mkindo mkoani Morogoro. Aidha, katika mazungumzo hayo Balozi Andayane alitoa taarifa kuwa serikali ya Indonesia imeisaidia Tanzania matrekta pamoja na vifaa vyake. Tayari Wizara ya Kilimo imeshughulikia uingizaji wa matrekta hayo.

Kwa upande wake, Balozi Mbelwa Kairuki aliishukuru serikali ya Indonesia kupitia Mkurugenzi huyo kwa misaada mbalimbali wanayotoa kwa serikali ya Tanzania. Pia alishukuru serikali ya Indonesia kwa kuialika Serikali ya Tanzania katika maadhimisho ya miaka 60 ya ushirikiano kati ya bara la Afrika na Asia zilizofanyika Jakarta na Bandung mwishoni mwa mwezi wa nne mwaka 2015.

No comments:

Post a Comment