Foreign Exchange Rates

DStv Advert_090724

DStv Advert_090724

SBT Tanzania Advert_291123

Thursday 14 May 2015

BENKI YA NMB YATOA MSAADA KWA HOSPITALI YA RUFAA DODOMA

Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Kapteni Mstaafu, Chiku Galawa (wa tatu kulia) akipokea sehemu ya shuka 422 na godoro 22 yenye thamani ya shilingi Milioni 10 kutoka kwa Meneja wa Benki ya NMB Kanda ya Kati, Gabriel ole-Loibanguti (kushoto). Vifaa hivyo vilitolewa na Benki ya NMB kwaajili ya hospitali ya rufaa ya Mkoa wa Dodoma katika hafla iliyofanyika kwenye kilele cha siku ya wauguzi duniani Dodoma.
Meneja wa Benki ya NMB Kanda ya Kati, Gabriel ole-Loibanguti (watatu kushoto), akikabidhi sehemu ya magodoro 22 na shuka 422 vyote vikiwa na thamani ya shilingi Milioni 10 kwa Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Kapteni Mstaaafu, Chiku Galawa zilizotolewa na NMB kwaajili ya hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Dodoma. Makabidhiano hayo yalifanyika kwenye kilele cha siku ya wauguzi duniani. Kulia ni Muuguzi Mkuu wa hospitali ya Dodoma, Anatolia Mkindo na kushoto ni Mganga Mkuu wa Hopsitali ya rufaa ya Mkoa wa Dodoma, Ezekiel Mpuya.
Benki ya NMB, imetoa msaada wa vifaa mbalimbali kwa hospitali ya rufaa ya Mkoa wa Dodoma vyenye thamani ya shilingi milioni 10 ikiwa na lengo la kusaidia uboreshaji wa huduma katika hospitali hiyo kubwa kwa mikoa ya kanda ya kati – Singida na Dodoma.

Baadhi ya vifaa vilivyotolewa ni magodoro 22 na mashuka 422 ambayo kwa maelezo ya Mganga Mkuu wa hospitali hiyo, Dr Ezekiel Mpuya vitasaidia sana kuweka mazingira rafiki kwa wagonjwa wanaolazwa hospitalini hapo hususani akina mama wajawazito na watoto.

No comments:

Post a Comment