Na Bakari Issa,Dar es Salaam.
Benki ya Biashara ya DCB imetoa msaada wa Kompyuta kwa Chuo cha Maendeleo ya Wananchi Arnautoglu kilichopo Manispaa ya Ilala,kwa lengo la kutoa elimu katika Chuo hiko chenye wanafunzi wenye ulemavu.
Akizungumza wakati wa hafla ya kukabidhi msaada huo wa Kompyuta kwa Chuo hicho, Naibu Waziri wa Maendeleo ya Jamii Jinsia na Watoto, Mhe. Dkt. Pindi Chana amesema umuhimu wa Vyuo hivi unatokana na lengo la kuanzishwa kwake ambalo ni kutoa maarifa na stadi zitakazowawezesha wananchi kujiajiri, kujitegemea ili kuondokana na ujinga, umaskini na maradhi hatimaye waweze kuchangia kuinua uchumi wa taifa.
Pia, Dkt. Chana amewahasa wazazi kuacha kuwaacha watoto wao kukaa nyumbani bila kujishughulisha na shughuli yeyote pindi wanapomaliza masomo yao na badala yake kuwashughulisha watoto hao ili kujiepuka kujiingiza kwenye makundi yasiyofaa.
Kwa upande wake, Meneja Masoko na Maendeleo ya Bidhaa wa DCB Commercial Bank, Bw.Boyd Mwaisame amesema Benki imekabidhi msaada huo kutokana na kuguswa na matatizo mengi yanayojitokeza katika jamii likiwemo la ukosefu wa vitendea kazi kwa watoto wenye Ulemavu.
Naye, Mkuu wa Chuo hicho, Bi. Pulcheria M. Ndamgoba ametoa shukrani kwa msaada huo wa Kompyuta katika Chuo hiko na kuahidi kukitumia vizuri katika kutoa elimu chuoni hapo, huko Kiongozi wa Wanafunzi wa Chuo hicho, Ridhwan Omary akitoa msisitizo kwa Benki hiyo kuwasaidia kujengea viwanja vya michezo.
No comments:
Post a Comment