Foreign Exchange Rates

DStv Advert_090724

DStv Advert_090724

SBT Tanzania Advert_291123

Tuesday 21 April 2015

BENKI YA CBA YAKABIDHI HUNDI YA SHILINGI MILIONI 5 KWAAJILI YA UJENZI WA HOSTELI YA WASICHANA SHULE YA SEKONDARI KIFARU MWANGA

Meneja masoko wa benki ya CBA Tanzania, Solomon Kawishe (kushoto), Meneja masoko Moshi Eliud Marko (katikati) wakimkabidhi Mwalimu mkuu wa shule ya sekondari ya Kifaru, Abdallah Mwomboke iliyopo katika kijiji cha Kituri kata ya Kileo wilaya ya Mwanga mkoani Kilimanjaro hundi ya shilingi Milioni tano yenye thamani ya zaidi ya mifuko 300 ya saruji kwa ajili ya ujenzi wa Hosteli ya wasichana katika shule hiyo, msaada huo ni sehemu ya kamapeni ya Book by Book inayoendeshwa na benki ya CBA ikilenga kusaidia serikali katika juhudi za Elimu (Picha na Pamela Mollel wa Jamiiblog).
Meneja masoko wa Benki ya CBA Tanzania Solomon Kawishe akizungumza na wanafunzi (hawapo pichani) kuhusu nia yao ya kuwasaidia msaada huo wa saruji kwa ajili ya kujenga hosteli ni kutokana na idadi ya wanafunzi 944 kuwa na changamoto kubwa ya ufaulu hasa jinsia ya kike huku akiwaasa wanafunzi hao kuwa Elimu ndio urithi pekee wa kuweza kuharakisha maendeleo Tanzania hivyo jamii inategemea kupata watu muhimu wakuwasaidia kama madaktari, wafanyakazi wa mabenki na hata walimu wa kuendeleza elimu.
Meneja masoko wa Benki ya CBA Moshi, Eliud Marko akiwa anasisitiza wadau mbalimbali wa makampuni makubwa kujitokeza kusaidia kuinua Elimu ili kupunguza umaskini nchini.
Mwalimu mkuu wa shule ya sekondari ya Kifaru, Abdallah Mwomboke iliyopo katika wilaya ya Mwanga mkoani Kilimanjaroakiwa anatoa neno lake la shukrani kwa Benki ya CBA kwa kufika na kuguswa kusaidia hosteli ya wasichana katika shule hiyo kutokana na wengi wameshindwa kuendelea na masomo shuleni baada ya kuingizwa katika mahusiano na wanaume hali ambayo inawawia vingumu kuweza kumudu masomo.

No comments:

Post a Comment