Foreign Exchange Rates

DStv Advert_090724

DStv Advert_090724

SBT Tanzania Advert_291123

Wednesday, 18 February 2015

WAZIRI WA ARDHI, NYUMBA NA MAENDELEO YA MAKAZI NA UJUMBE WAKE ZIARANI NCHINI SINGAPORE

Ujumbe wa Tanzania chini ya Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi ukionyeshwa namna Serikali ya Singapore inavyoratibu upatikanaji wa nyumba kwa wananchi wake ulipotembelea Bodi ya Maendeleo ya Nyumba ya Singapore jana. Jumla ya nyumba 900,000 zimeshajengwa na Bodi hii na kupatiwa wananchi kupitia ruzuku ya serikali na nyumba 50,000 zinapangishwa kwa wananchi kwa kodi isiyozidi asilimia 5. Taifa la Singapore lina watu milioni 5.4 na asilimia 99 ya watu wa nchi hiyo wamewezeshwa kumiliki nyumba.
Ujumbe wa Tanzania ukitembelea vyumba vya mfano vya ukubwa tofauti vinavyojengwa na Bodi ya nyumba ya Singapore kwa ajili ya kuuzia au kupangisha wananchi kulingana na uwezo, mahitaji na ukubwa wa familia. Vyumba hivi vipo Makao Makuu ya Bodi ya Nyumba ya Singapore ambavyo ni kivutio kwa wageni wanaotembelea jengo hilo kujifunza namna ya kuhudumia watu wa kada mbalimbali wanaohitaji nyumba.
Ujumbe wa Tanzania ukielezwa historia ya hatua mbalimbali za maendeleo ya sekta ya nyumba nchini Singapore walipotembelea Bodi ya Maendeleo ya nyumba nchini humo jana.
Ujumbe wa Waziri Lukuvi ukiwa katika mji wa kisasa wa Punggol wenye ukubwa wa kilomita za mraba kumi ambao una nyumba zilizojengwa na Bodi ya Maendeleo ya Nyumba Singapore kwa ajili ya wananchi wa kipato cha kati na chini. Katika eneo hili nyumba zimewekewa miundombinu ya kisasa na zina watu wanaofikia 250,000. Hapa ni ghorofa ya pili ya jengo mojawapo lililojengwa katika mji huu wa kisasa.
Majengo ya kisasa katika mji wa Punggol nchini Singapore yanayokaliwa na wananchi waliouziwa na Bodi ya Nyumba ya Singapore kupitia mifuko ya jamii na ruzuku ya serikali .

Ujumbe wa Tanzania ukiwa eneo la Punggol Point Park ambalo ng’ambo yake ni bandari ya nchi ya Malaysia inayopakana kwa karibu na nchi ya Singapore.
Bofya hapa kwa picha zaidi

No comments:

Post a Comment